Uvumilivu na Faraja
Yohana mbatizaji, alipotokea kama mtangulizi wa Masihi, alitikisa taifa. Kutoka mahali hadi mahali, hatua zake zilifuatwa na makundi makubwa ya watu wa kila cheo na sehemu zote. Lakini alipokuja Yule ambaye alikuwa akimshuhudia, yote yalibadilika. Makutano walimfuata Yesu na kazi ya Yohana ikaonekana ikielekea mwisho kwa haraka.
Lakini imani yake haikuyumba.
"Yeye hana budi kuzidi" alisema "bali Mimi kupungua" Yohana 3:30.
Muda ukapita na ufalme ambao Yohana aliutazamia haukuanzishwa. Katika gereza la Herode, akitengwa na hewa iletayo uhai na pasipo uhuru, alisubiri akikesha.
Hakukuwepo na matumizi ya silaha, wala kuvunjwa kwa milango ya gereza; bali uponyaji wa wagonjwa, kuhubiriwa kwa Injili, kuinuliwa kwa Roho za watu, vilishuhudia utume wa Kristo.
Akiwa peke yake gerezani, akiona njia yake, kama ile ya Bwana wake, ilikoelekea, Yohana akaikubali amana, ushirika na Kristo katika Kafara.
Mungu atujalie kumwandama hata pale ambapo taraja ya mioyo yetu inaonekana kuchelewa au kutotimia kabisa.
Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv
Barikiwa
Post a Comment