Amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

Alhamis 23/07/2020

#YESU_NA_RAFIKI_ZAKE_WAKIWA_BETHANIA*

*Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro.* Yohana 11:5

💎 Kulikuwa na kaya moja ambayo alipenda kuitembelea—nyumbani kwao Lazaro, na Mariamu, na Martha; kwa kuwa katika angahewa ya imani na upendo roho yake ilikuwa na pumziko. Miongoni mwa wanafunzi imara sana wa Kristo alikuwamo Lazaro wa Bethania. Tangu walipokutana kwa mara ya kwanza imani yake kwa Kristo ilikuwa na nguvu; upendo wake kwake ulikuwa ni wa kina, naye alipendwa sana na Mwokozi.

💎 Ilikuwa ni kwa ajili ya Lazaro muujiza wa Kristo ulio mkuu kuliko yote ulifanywa. Mwokozi aliwabariki wote waliotafuta msaada Wake; Yeye anawapenda familia yote ya wanadamu; lakini kwa wengine amefungwa kwa ushirika wa namna ya pekee. Moyo wake uliunganishwa na kifungo chenye nguvu cha upendo kwa familia hiyo iliyokuwa Bethania, na kwa mmoja wao kazi yake ya ajabu sana ilitendwa. 

💎 Nyumbani mwa Lazaro, mara nyingi Yesu alipata pumziko. Mwokozi hakuwa na nyumba Yake mwenyewe; Alikuwa akitegemea ukarimu wa marafiki na wanafunzi wake; na mara nyingi, akiwa amechoka, akiwa na kiu ya ushirika wa wanadamu, alifurahi kukimbilia kaya hii ya amani, mbali na tuhuma na wivu wa Mafarisayo wenye hasira. Hapa alipata ukaribisho wa dhati, urafiki safi, mtakatifu. Hapa angeweza kusema kwa usahili na uhuru kamili, akijua kuwa maneno yake yangeeleweka na kuthaminiwa. 

💎 Mwokozi wetu alifurahia nyumba tulivu na wasikilizaji wenye kuvutiwa; Alitamani sana wema wa kibinadamu, uungwana, na upendo. Wale ambao walipokea mafundisho ya kutoka mbinguni aliyokuwa tayari kila wakati kuyatoa walibarikiwa sana.... 

🔘 *Umati wa watu walikuwa wazito wa kusikia, na katika nyumba ya kule Bethania Kristo alipata pumziko kutoka katika mapambano ya kuchosha ya maisha ya jamii. Hapa katika mahojiano ya faragha aliwafungulia wasikilizaji wake kile ambacho hakujaribu kuwaambia umati uliochanganyika. Hakuhitaji kuzungumza na rafiki zake kwa mifano.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv

No comments