lesoni"nguvu ya roho mtakatifu"

*LESONI LEO.*

Alhamisi 30 Julai 2020.

*SOMO: NGUVU YA ROHO MTAKATIFU INAYOBADILISHA MAISHA.*

Kujifunza kitabu cha Matendo kwa uangalifu kunamfunua Mungu kupitia Roho Mtakatifu anayefanya miujiza katika maisha ya watu. Kitabu cha Matendo kinafundisha juu ushindi wa injili dhidi ya utamaduni wa watu, uwezo wa injili wa kubadili tabia zilizojengeka na kukumbatiwa kwa muda mrefu, na kuwafundisha wanadamu wote juu ya neema na ukweli wa Kristo. Roho Mtakatifu anakutana na watu mahali walipo, lakini hawaachi pale. Katika uwepo Wake, wanabadilishwa. Maisha yao yanageuzwa na kuwa tofauti. 

*Soma Matendo 16:11–15, 23–34; Matendo 17:33, 34; na Matendo 18:8. Hivi ni visa vichache tu vya uongofu katika Biblia. Visa mbalimbali vinatufundisha nini kuhusu uwezo wa Mungu wa kubadili maisha ya watu wa kila aina na walio mazingira mbalimbali?*

Tofauti za watu zilikuwa kubwa ajabu. Lidia alikuwa mwanamke mfanyabiashara wa Kiyahudi aliyefanikiwa sana, mkuu wa gereza la Filipi alikuwa mtumishi wa serikali ya Kirumi wa daraja la kati. Roho Mtakatifu anaweza kuzifikia safu zote za jamii. Nguvu Yake inayobadilisha maisha inaweza kuwafikia wanaume na wanawake, matajiri na maskini, wasomi na wasiokuwa wasomi. 

Wahusika wawili wa mwisho kwenye orodha yetu ni wa kushangaza pia. Matendo 7:34 huzungumzia kuongoka kwa Dionisia Mwareopago. Waareopago wa Atheni walikuwa sehemu ya wanasheria mashauri wa majaji waliosikiliza kesi mahakamani. Walikuwa watu mashuhuri walioheshimika katika jamii ya Kiyunani. 

Kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, huduma ya mtume Paulo iliwafikia hata watu wa daraja la juu katika jamii. Krispo (Matendo 18:8) alikuwa mtawala wa sinagogi la Kiyahudi. Alikuwa kiongozi wa dini aliyezama katika elimu ya Kiyahudi ya Agano la Kale, na Roho Mtakatifu aliingilia kati na kubadilisha maisha yake. 

Mifano hii ya kihistoria hudhihirisha kuwa tunapomshuhudia Kristo na kuwahubiri wengine Neno Lake, Roho Mtakatifu anafanya mambo makubwa katika maisha ya watu wa kila namna na wenye mazingira, utamaduni, elimu, na imani za aina mbalimbali. Hatuwezi na wala hatupaswi kubahatisha juu ya wale tunaoweza au ambao hatuwezi kuwafikia. Kazi yetu ni kumshuhudla kila mmoja ambaye analetwa maishani mwetu. Bwana atamalizia yaliyobaki.

*Kifo cha Kristo kilikuwa cha ulimwengu wote; maana yake ni kuwa, kilikuwa ni kwa ajili ya kila mwanadamu. Ukweli huu muhimu unapaswa kutufundisha nini kuhusu jinsi ambavyo hatupaswi kumchukulia mtu ye yote kuwa nje ya tumaini la wokovu?*
🙏🙏🙏🙏

Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv

No comments