amka na Bwana

_*KESHA LA ASUBUHI*_

_JUMAMOSI, JULAI 18_

```SOMO: HEBU WAGENI WASHIRIKI KATIKA IBADA YA FAMILIA```

_*Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.*_
_1 Petro 2:9_


```📖Kwa namna fulani baba ni kuhani wa kaya, akiweka juu ya madhabahu ya familia sadaka ya asubuhi na ya jioni. Lakini mke na watoto wanapaswa kuungana kwenye sala kwa wimbo wa sifa. Asubuhi kabla hajaondoka nyumbani kwa ajili ya kazi zake za kila siku hebu baba awakusanye watoto wake kumzunguka na, kwa kusujudu mbele za Mungu, awaweke chini ya utunzaji wa Baba aliye mbinguni. Baada ya masumbuko ya siku kupita, hebu familia iungane katika kutoa sala ya shukurani na kuinua wimbo wa sifa, kwa kukiri utunzaji wa Mungu wakati wa mchana.... Usikose kukusanya familia yako kuzunguka madhabahu ya Mungu.```


 ```📖Katika juhudi zetu kwa ajili ya faraja na furaha ya wageni hebu tusiache kuangalia wajibu wetu kwa Mungu. Saa ya sala haipaswi kupuuzwa kwa sababu yoyote ile. Msizungumze na kufurahi pamoja hadi wote wamechoka kiasi cha kutokufurahia kipindi cha ibada. Kufanya hivyo ni kumtolea Mungu dhabihu kilema. Katika saa za mapema jioni, wakati tunapoweza kuomba bila haraka na kwa kuelewa, ndipo inatupasa kuwasilisha maombi yetu na kupaza sauti zetu kwa sifa za furaha na kushukuru.``` 


```📖 Hebu wote wanaowatembelea Wakristo waone kuwa saa ya sala ndio ya thamani na takatifu mno, saa ya furaha kuliko zote za siku. Vipindi hivi vya ibada huweka mvuto wenye kutakasa, unaoinua kwa wote wanaovishiriki. Vinaleta amani na pumziko tamu kwa roho. ```


```📖 Taa, hata ikiwa ndogo kiasi gani, ikiwa itadumishwa kuwaka, inaweza kuwa njia ya kuwasha taa zingine nyingi.... Fursa za ajabu ni zetu kupitia katika utumiaji kwa uaminifu wa fursa za nyumba zetu wenyewe. Ikiwa tutafungua mioyo yetu na nyumba zetu kwa ajili kanuni takatifu za maisha, tutakuwa mifereji kwa ajili ya mikondo ya nguvu iletayo uzima. Kutoka katika nyumba zetu itatiririka mito ya uponyaji, ikileta uhai, na uzuri, na uwezo wa kuzaa pale ambapo kwa sasa pana ukame na uchache.```

No comments