kijionesha kwetu kwamnyima muhitaji chakula
Kupenda kujionesha huzalisha utumiaji mbaya wa pesa, na kwa vijana wengi huzima ile ari ya kuishi maisha ya kiungwana.
Hivyo, hutafuta pesa ili kukidhi uchu wao wa mavazi.
Na kwa uchu huo wasichana wengi hudanganywa na kuharibikiwa.
Wengi hawajali hata kama vazi linawapendeza kiasi gani au hata liwe zuri sana, mtindo ukibadilika, lazima litarekebishwa ama kutupiliwa mbali.
Hata siku na huduma zake za ibada haziko salama kutokana na utawala wa mitindo.
Matajiri wana uchu wa kushindana katika mitindo yao inayobadilika badilika daima; watu wa kati na tabaka la maskini wanakazana kufikia kiwango kilichowekwa na wale walio juu yao. Pale ambapo uwezo au nguvu zimepungua, na bado shauku ya kuishi maisha ya juu ni kubwa, mzigo huwa hauvumiliki.
NB: Kila shilingi iliyotumiwa ovyo kwa kujionesha, mwenye kuzitumia amejinyima uwezo wa kuwasaidia wenye njaa, kuwavisha walio uchi, na kuwafariji wenye huzuni.
Post a Comment