mjue msengenyaji
Katika maandiko, wasengenyaji wamewekwa pamoja na "wamchukiao Mungu," "wanaobuni uovu," pamoja nao "wasio na upendo, wenye chuki, wasio na huruma," "walio na wivu, wauaji, wadanganyifu, wenye shari."
"Ni hukumu ya Mungu kuwa hao wafanyao hayo wapaswa kifo."
Rum. 1:30, 29, 32.
Yeye ahesabiwaye na Mungu kuwa mwananchi wa Sayuni ni yule "anenaye ukweli moyoni mwake,"
"asiyesengenya kwa ulimi," "Wala hakumsengenya jirani yake." Zab. 15:2, 3.
"Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge, na mishale, na mauti; ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake, na kusema, je! sikufanya mzaha tu!" Mit. 26:18, 19.
Kinachopelekana kwa karibu sana na usengenyaji ni kupenyezwa kwa uchongezi, vijembe vinavyoletwa na uongo, ambao kwa huo wasiosafi mioyoni wanatafuta kupenyeza uovu ambao hawathubutu kuutoa hadharani. Mwelekeo wowote wa mazoea haya vijana wanapaswa kufundishwa kuyaepuka kama waepukavyo ukoma (au ukimwi leo).
Post a Comment