Shirika la kuzia majanga la kisabato lazidi kufanya kazi vizuri


Shirika la kiadiventista wasabato  ADRA :-Tanzania limezidi kufanya kile kinachotajwa na Biblia kama “dini ya kweli na safi” kwa kuwafikia watu mbalimbali wanaokumbwa na majanga.

Taarifa iliyotolewa leo kwenye mikutano ya GAiN inayoendelea jijini Arusha na kiongozi wa ADRA Tanzania, Samwel Oyertey imeonesha ni kwa kiasi gani shirika hilo linawagusa watu wengi kupitia misaada yake.

Bwana Oyertey ametolea mfano wa msaada uliotolewa na ADRA wilayani Longido mkoani Arusha kwa kuifikia jamii ya kimasai punde baada ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwa kuhakikisha upatikanaji wa maji safi.


Picha kwa hisania ya ADRA TANZANIA
Mikutano hii inayofanyikia kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano (AICC) inatarajiwa kumalizika kesho siku ya Sabato. Hii ni mikutano inayojumuisha Union zote mbili ambapo viongozi wa kanisa kama wachungaji Mark Marekana na Godwin Lekundayo wamehudhuria.

WEKA MAONI YAKO HAPA

No comments