Mchungaji James Ng'ang'a awamwagia matusi maaskofu wake
Mchungaji maarufu nchini Kenya Ng’ang’a wa kanisa la Neno Evangelist Ministry amegonga vichwa vya habari kwa mara nyengine tena baada ya kutishia kufunga matawi ya kanisa lake la Neno Evangelism akidai kwamba maaskofu hawamuheshimu mke wake. Katika kanda ya video iliosambaa katika vyombo vya habari , anaonekana akiwakaripia maaskofu kwamba atawafurusha wote iwapo hawataheshimu onyo lake akidai kuwa matawi hayo yamekuwa vibanda.
Iwapo munataka kujiita maaskofu, munahitaji kufikiria kule mulikotoka, ni vipi munajigamba mbele yangu na mulikuja kwangu na umaskini…nitawafukuza nyie nyote… takataka”, aliendelea.
Post a Comment