Mke wa Gwajima Grace ameamua kutoa yake kutoka moyoni juu ya mumewe



Je ukweli ni upi kuhusu hii video???
Mei 8 mwaka huu Grace, mke wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima alizungumzia kuhusu video hiyo inayomuonyesha mtu mwenye sura kama ya mumewe, akisema si yeye kwa kuwa anamfahamu vyema.

Grace alisema anafahamu ukweli wa video hiyo na kamwe haiwezi kumyumbisha kwa maelezo kuwa anamfahamu vyema mumewe.

“Mimi ni kama simba, ukweli naufahamu, namfahamu mume wangu na kumuamini na ukweli huo hakuna mtu anayeweza kuubadilisha.”

“Nipo pamoja na yeye na nitasimama na yeye. Mungu akiwa upande wetu hakuna atakayeweza kuwa juu yetu,” alisema Grace.

Wakati Grace akizungumza mamia ya waumini wa kanisa hilo walionekana wakimshangilia na kuruka ruka kwa furaha.
Je ukweli upo wapi!?
Mimi sijui

1 comment: