Rose Muhando Aweka wazi mahusiano yake na Kijana mkenya

@rose_muhando & @Stephen_kasolo

Muimbaji wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando ameeleza uhusiano wake na kijana kutoka Kenya aitwaye Steven Kasolo, ambaye ndiye anayeishi naye kwa sasa nchini humo.

Akizungumza na moja ya mtandao kutoka nchini humo, Rose amesema kuwa, kukutana kwake na kijana huyo ni kusudi la Mungu na hakuna kitu kingine zaidi ya hilo na hawana uhusiano wa kimapenzi kama watu wanavyodai.

"Kasolo alinichukua kama mama wa huduma na hivyo upendo wake kwangu ni kama mama yake, na nilikubali kuishi naye ili kutimiza kusudi la Mungu", amesema Rose Muhando.

Ameongeza kuwa, "Watu wanapotuona wawili wajue kuwa ni kusudi la Mungu, nafanya kwaajili yake na ninafanya kwa upande wangu, jamii naomba inielewe kwenye hili".

Rose Muhando amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya taarifa zilizoibuka kupitia mitandao ya kijamii zilizodai kuwa wawili hao walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi.

No comments