"Sitakufa" mchungaji Lusekelo alisema

Mchungaji wa kanisa la Maombezi GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako, amefunguka juu ya taarifa za kuzushiwa kifo, na kusema kuwa yeye hajafa.

Mchungaji Lusekelo amefunguka hayo kwenye video moja inayomuonesha akiwa amekaa akionekana na afya njema, na kusema kwamba yeye hajafa na wala haumwi.

“Eti nini!?, nimekufa!?. Mimi sijafa, wala siumwi hata mafua, niko mzima, watu wangu wote muwe na amani, eti nini!!? nimekufaa!!. Nitabaki kuwa juu, nitabaki kileleni”, amesema Mchungaji Lusekelo.

Picha inayomuonesha Anthony Lusekelo akiwa amedhoofu

Mchungaji Lusekelo alimalizia taarifa hiyo huku akipiga kionjo cha Piere Mzee wa Liquid, huku akifurahi.

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikisema kuwa Mchungaji huyo hali yake ni mbaya kiafya, huku zingine zikisema kuwa ameshafariki dunia.

No comments