Morice Chukwu kutua Simba kutoka Rivers United
MORICE CHUKWU Kiungo mkabaji kutoka Rivers United ya NIGERIA 🇳🇬 amesajiliwa na Simba SC na atatangazwa hivi karibuni.
CHUKWU miaka 27 amewahi pia kuchezea Klabu cha AKWA SPORT pia cha Nigeria.
Ujio wake utamfanya Mnigeria mwingine VICTOR AKPAN kupelekwa kwa mkopo ili kutoa nafasi kwa Chukwu.
Akpan aliyesajiliwa kutoka Coastal Union msimu huu ameshindwa kushawishi kwa Kocha Zoran kwamba ni kiungo anaeweza kuivusha Simba akicheza mbele ya mstari wa mabeki.
NB: Kuna Wachezaji wengine 2 wa ndani wanapelekwa kwa mkopo kabla ya dirisha la usajili kufungwa
Post a Comment