Mfahamu zaidi Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Solomon Mukubwa
Solomon Mukubwa ni mwimbaji wa nyimbo za injili; hasa kwa lugha ya Kiswahili.
BW Solomon Mukubwa ni mwimbaji wa nyimbo za injili; hasa kwa lugha ya Kiswahili.
Anatoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) japo anaishi nchini Kenya.
Mwanamuziki huyo anafahamika kwa wimbo maarufu wa ‘Mfalme wa Amani’.
Mukubwa, ni msanii aliyepitia changamoto tele akiwa mdogo ingawa ndoto zake za kuwa mwimbaji hazikufifia.
Akiwa na umri wa miaka 12, alipata matatizo ya uvimbe wa mkono wa kushoto.
Anasema uvimbe huo ulikuwa wa ajabu kiasi kwamba hakuna aliyefahamu chanzo chake. “Niliugua kwa muda wa miaka mitatu, wazazi wangu walihangaika kunipeleka katika hospitali mbalimbali na hata kwa waganga wa kienyeji bila mafanikio,” anaeleza.
Anaendelea kusimulia kuwa karibu na kwao, ilizinduliwa hospitali moja ya Wazungu ambapo baada ya kukaguliwa madaktari waliomshughulikia walipendekeza mkono huo ukatwe ili kunusuru maisha yake.
Aidha, madaktari wenye ujuzi wa hadhi ya juu walishindwa kuokoa mkono huo ikiwa ni waganga.
“Nilipoteza mkono wangu kwa hali hiyo,” Bw Mukubwa anafichua.
Kulingana na mwanamuziki huyo ni kwamba hakuna aliyejua hasa uvimbe huo umetokana na nini.
Baadaye ilifichuka mamake wa kambo ndiye alimroga na kumsababishia tatizo hilo.
“Baadaye mamangu wa kambo alikiri na kueleza ukweli nilipopona mkono,” anasema.
Hata hivyo, anasema alimsamehe baada ya kuokoka. Mama huyo wa kambo pia aliokoka kutokana na pigo kali alilopitia mwanawe baada ya jicho lake kuponza. “Mtoto wake alikuwa akicheza na kaa la moto lililomuingia kwenye jicho na kuharibika kabisa,” anaeleza.
Ni kutokana na masaibu hayo ambapo Mukubwa alizamia safu ya uanamuziki na kutunga wimbo ‘Mfalme wa Amani’ uliolenga kumtukuza na kumshukuru Mungu baada ya kumuepushia kifo. “Wimbo wangu wa ‘Mfalme wa Amani’ niliuimba baada ya kupitia shida hizo. Albamu yangu ya kwanza niliipa jina ‘Mungu mwenye Nguvu’ na kuna maneno niliyoweka kwenye kibao hicho kwamba ukiwa na shida usiende kwa waganga wa dunia. Mwite Mungu ambaye ni Mfalme wa amani, yeye ndiye hujibu maombi ya kila mtu,” anafafanua.
Mukubwa ambaye pia ni mchungaji ni mwanamuziki mwenye bidii mithili ya mchwa, na anasema kuwa kipaji chake amepewa na Mungu.
Anasema nyimbo zake nyingi alijifunza kwa waimbaji wa injili Tanzania.
Aliondoka DRC 2003 na kuelekea nchini Uganda. Miaka mitatu na nusu baadaye alipatana na mwanamuziki Angela Chibalonza, ambaye kwa sasa ni marehemu na kwamba ndiye alimpokea jijini Nairobi.
“Angela Chibalonza ndiye alininoa katika uimbaji licha ya kwamba nilipokutana naye nilikuwa katika harakati za kurekodi albamu yangu ya pili ya Sijaona Rafiki kama Yesu,” anasema. Anaongeza kuwa ufanisi wake katika sanaa ya uimbaji ulifanikishwa na Bi Chibalonza.
Mbali na albamu Mungu mwenye Nguvu na Sijaona Rafiki kama Yesu, Mukubwa pia ana albamu zingine kama Kwa Utukufu wake Mungu, Sifa za Mungu, Kwa Utukufu wake Bwana, na Penina na Anah.
Chanzo;-Swahilihub

Post a Comment