Utafiti;-Wanawake ambao huenda Kanisani huishi zaidi

Wakristo wengi huenda kanisani kulishwa chakula cha kiroho na kuimarisha imani yao. Ikiwa unaenda kanisani mara moja kwa wiki ikiwa wewe ni mwanamke, basi kuna habari njema kwako.

Utafiti uliochapishwa na Mail Online Mei 16, 2016 na ullioonekana na TUKO.co.ke ulionyesha kuwa wanawake ambao huenda kanisani mara moja kwa juma wana uwezo wa kupunguza hatari ya kufariki kwa asilimia 25.

Habari Nyingine: Akothee amshambulia shabiki aliyedai hajavaa chupi

Utafiti huo uliofanywa na Chuo cha Harvard T.H. Chan School of Public Health Marekani ulichanganua data kutoka kwa watu 75,000, wote wanawake wauguzi wa umri wa makamo.

Utafiti huo kati ya 1992 na 2002 ulionyesha kuwa wanawake walioenda kanisani mara moja kwa wiki walikuwa na uwezo wa kupunguza hatari ya kufa kwa asilimia 33, wakilinganishwa na wale ambao hawakwenda kanisani.

Kwa muda wa miaka, wahusika katika utafiti huo walijibu maswali kuhusiana na ikiwa walienda kanisani au la, “Wanawake waliofika kanisani chini ya mara moja kwa wiki walikuwa na uwezo wa kuishi zaidi wa kati ya asilimia 26 na 13,” alieleza Prof Tyler J. VanderWeele, chuoni humo.

Hii ni kumaanisha kuwa, walioenda kanisani mara nyingi walikuwa wamepunguza magonjwa ya moyo na kansa na ndio maana walikuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuishi wakilinganishwa na wale ambao hawakuenda.

Hii ni kutokana na matumaini maishani, kwa kukabiliana na athari za shinikizo na mfadhaiko, watafiti hao walisema.

Source;-Tuko.co.ke

No comments