Kijana alishitaki kanisa kwa kupewa masharti magumu ya kufanya ndoa




Mwanaume mmoja ameshitaki kanisa moja nchini Uganda akipinga kanuni za utaratibu wa kufunga ndoa akieleza kuwa zinakwenda kinyume na katiba.

Michael Aboneka amepeleka kesi hiyo katika mahakama ya katiba mjini Kampala kulishtaki kanisa la Watoto Church wakati waumini wengine wa kanisa hilo wakiunga mkono taratibu za kanisa lao.

Michael Aboneka amesema kuwa Watoto Church, linawanyima vijana wengi haki yao ya kikatiba ya kufunga ndoa na wapenzi wao baada ya kutimiza umri wa miaka 18 kama katiba ya Uganda inavyosema.

Ameeleza kuwa baada ya kuzisoma kanuni hizo za kufunga ndoa, ameona kuwa zinakwenda kinyume na katiba.

Kwanza wanasema nilazima upate barua kutoka kwa wazazi wa bibi harusi ambayo wanaita Baraka. Kwangu inakwenda na kinyume cha katiba kifungu 31 ya ndoa ya pili ni kukabidhi barua ya Dakitari ya majibu ya kupima virusi vya ukimwi kwa kanisa'.

'Nimekwenda hospitalini kupimwa na mchumba wangu tumepata majibu tunafahamu majibu ya kila mmoja wetu. Kwa hiyo mimi na mchumba wangu kukabidhi vipimo vya ukimwi kwa kanisa inavunja haki ya uhuru wa siri zetu, nimekuta ni kinyume na katiba'. amesema Aboneka.


Wabunge wapigana makonde Uganda
Aboneka ameongeza kuwa kununi nyingine ambazo anaziona kama kero ni kusubiri kwa mda wa miezi sita baada ya kuomba kufanya harusi na kulipa ada katika kanisa shilingi lakini nne na nusu za Uganda sawa na dola 130.

Lakini kwa waumini wa kanisa hilo wao waanasema hakuna tatizo.

'Ndio naunga mkono sheria na taratibu za kufunga ndoa katika kanisa ya watoto, kwa sababu kila jamii wana taraibu zao na sheria zinazowaongoza, amesema Vanesa Naluwoga.

'Hivyo nina unga mukono. Na mimi mwenyewe nilifunga ndoa tarehe 27 October 2012 kwa kupitia taratibu hizo zote tulizoambiwa', ameongeza Naluwoga.


Michael Aboneka ameongeza kusema kuwa siyo kanisa la watoto pekee lenye utaratibu huo bali makanisa mengi nchini yanafanya hivyo na anasema ameiomba mahakama ya katiba kuanza mara moja kusimamisha kanuni hizo na anatarajia wiki hii mahakama inaweza kutowa jibu.

Aboneka amesema kuwa siyo kwamba ana chuki na kanisa la watoto, ila ni kusaidia vijana wengi ambao wameshindwa kufunga ndoa zao ili mahakama ya katibu itowe ufumbuzi wa swala hilo.

No comments