Hii ni kwa Wakristo wa kike(MAVAZI),usiache kuisoma hii
MWENENDO WA MKRISTO WA KIKE
Wakristo wa kike hawapaswi kujipamba kwa mambo ya nje, ambayo hayana faida yoyote katika wokovu wao. Kujipamba kwao kunatakiwa kuwa kujipamba kwa kutunza maagizo ya Mungu, wala si kujipamba kwa mavazi ya gharama, mafupi, na mapambo mengine yeyote yale. Biblia inafundisha njia nzuri ambayo wanawake wote ambao wanahitaji kumpendeza Mungu na kutii Neno lake lazima waifuate. Mwanamke yeyote aliye na Roho wa Mungu baada ya kusoma mafungu ya Biblia yafuatayo atajua ya kuwa Biblia kwa hakika inakataza mwanamke wa Kikristo kujipamba mapambo ya nje ambayo hayana faida yoyote kwa wokovu mtu.
1 Timotheo 2:9-10 inasema, “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.”
“Mavazi ya kujisitiri” sio “nguo za thamani” kama Paulo anavyothibitisha katika fungu hilohilo, mavazi ya kujisitiri ni mavazi ya adabu ambayo yanafunika vizuri mwili wa mwanamke, neno la kigiriki kwa ajili ya “mavazi ya kujistili” ni αἰδοῦς (aidous) ambalo linamaanisha “hali ya kuona aibu”, Thayer’s Greek Lexicon inasema, αἰδοῦς hutumika kumwonyesha “mtu mwema kutoka katika matendo yasiyostahili [ya aibu]”, na hivyo Paulo alikuwa anawaagiza wanawake kuvaa mavazi ambayo hayaleti aibu, mavazi marefu na yenye heshima. Pia akataza kusuka nywele, kuvaa mavazi ya thamani, dhahabu, lulu au mapambo mengine ya kimwili, bali kujipamba kwao kuwe katika kuenenda kwa kiasi na adabu, na matendo mema; kwani mambo hayo ndiyo yawapasayo kufanya wanawake wote wamchao Mungu. Mtume Petro naye pia anatuambia…
1 Petro 3:2-4 “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.”
Petro kama vile Paulo kwa kuwa waliongozwa na Roho moja, naye anakataza kujipamba kwa “kusuka nywele”, “kujipamba kwa mavazi”, na “kujitia dhahabu”; heri kujipamba kwa kufanya maagizo ya Mungu na kufanya matendo mema; maana hayo ndiyo mapambo yanayokubalika mbele za Mungu, Petro anatuambia zaidi kwamba hayo ndiyo mapambo waliyojipamba wanawake wa zamani waliomcha Mungu. Mwanamke hatakiwi kujipamba kwa “kusuka nywele”, au “kujipamba kwa mavazi”, na “kutoboa masikio” au “kupaka rangi kwenye makucha” au “kuweka alama yoyote katika mwili”
Walawi 19:28 “Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana.”
Isaya katika sura ya 3 wakati alipokuwa akitabiri kuhusuriwa kwa Yerusalemu, alionyesha anasa ambazo watu wa Yerusalemu walikuwa wakifanya, kisha akatabiri kwamba anasa kama hizo zingekuja kugeuka kuwa taabu. Fungu la 8 linasema, “Kwa maana Yerusalemu umebomolewa na Yuda wameanguka, kwa sababu ulimi wao na matendo yao ni kinyume cha Bwana, hata wayachukize macho ya utukufu wake. Matendo yao yalikuwa kinyume na Bwana, na je unajua kuwa pia wanawake wao walikuwa “wakisuka nywele” na kujipamba mapambo ya kimwili kama vile watu wa mataifa? Matendo hayo yalikuwa kinyume na Bwana, na katika fungu la 28 Isaya akatabiri juu yao kwamba kusuka kwao nywele kungekuja kugeuka kuwa upaa, anasema, “Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizosukwa vizuri, upaa; na badala ya kisibau, mavazi ya kigunia; na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri.”
Isaya 3:16-23 “Bwana akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienenda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao; Basi, kwa hiyo, Bwana atawapiga binti za Sayuni kwa pele za utosini, na Bwana ataifunua aibu yao. Siku hiyo Bwana atawaondolea uzuri

Post a Comment