Kosa sio la Askofu Shoo,bali ni Katiba ya KKKT ndio imemfunga
Katika siku za karibuni, tunashuhudia migogoro ikiibuka ndani ya sharika na dayosisi za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), huku mkuu wa kanisa hilo, Fredrick Shoo akibebeshwa lawama.
Lakini, ukitazama kwa undani, kiini si ukimya wa Askofu Shoo katika kuingilia migogoro hii, bali ni katiba ya KKKT ambayo imemfunga mikono yeye na halmashauri yake kuzisemea dayosisi hizi.
Bahati mbaya sana, hata baadhi ya wanahabari ambao walipaswa kuujulisha umma kwa usahihi, nao wameingia katika mkumbo wa kumuona mkuu wa KKKT kwamba anaweza kuingilia uendeshaji wa dayosisi.
Viongozi na vyombo vilivyoundwa kwa mujibu wa katiba za dayosisi zao visikimbie vivuli vyao katika kushughulikia matatizo yao. Mkuu wa Kanisa anaingiliaje wakati kila dayosisi ni mamlaka kamili?
Kwa sasa kuna migogoro ndani ya dayosisi mbili ambazo ni Dayosisi ya Kusini inayoongozwa na Askofu Isaya Mengele na Dayosisi ya Ziwa Tanganyika inayoongozwa na Askofu Ambele Mwaipopo.
Mgogoro ndani ya Dayosisi ya Kusini ulianza 2014 baada ya jimbo la Mufindi kujitenga na dayosisi na kukataa kuwa chini ya Askofu Mengele, kwa madai ya baadhi yao kudhalilishwa kwa kupelekwa polisi.
Lakini, mgogoro ndani ya Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, ulianza 2017 kati ya washarika wa Mpanda na uongozi wa dayosisi, ambapo washarika wanapinga kuhamishwa kwa mchungaji wao, Calvin Kessy.
Juzijuzi tu hapa katika usharika wa Sumbawanga mjini, kumetokea vurugu zilizosababisha Askofu Mwaipopo kupigwa mawe na akachukua hatua ya kuwafukuza washarika hao na kuwatenga kabisa.
Tunapotafakari chanzo cha migogoro hii, je, tunaweza kusema ni migogoro ya kanisa zima la KKKT au ni migogoro ndani ya dayosisi hizo mbili ambazo zina mamlaka kamili na Halmashauri zake.
Tujiulize, shutuma zinapaswa kuelekezwa kwa mkuu wa kanisa na Halmashauri yake au kwa maaskofu wa dayosisi hizo na vyombo vyake vya kikatiba kama halmashauri kuu ya dayosisi?
Sio rahisi kwa mtu kupata majibu sahihi bila kuufahamu vizuri muundo wa KKKT. Kwangu mimi hapa ndipo penye tatizo kwa wengi wanaotafsiri kuna mgogoro na Dk Shoo ameshindwa kuitatua.
Muundo wa KKKT ni tofauti sana na muundo wa makanisa mengine. Ni vema ikafahamika kuwa KKKT inaundwa na dayosisi zake na kila moja ina mamlaka kamili.
Kila dayosisi ni mamlaka yenye katiba yake iliyoanzishwa kisheria, na yenye kuongozwa na vyombo vyake vya kikatiba vikiwa ni mkutano mkuu na halmashauri kuu chini ya askofu kama mwenyekiti.
Kwa maana hiyo, mkuu wa KKKT hana mamlaka ya kuiamulia dayosisi yoyote mambo yake wala askofu wa dayosisi yoyote hawajibiki kwa mkuu wa Kanisa na Halmashauri Kuu ya Kanisa.
Mkuu wa Kanisa na halmashauri yake kuu wanayo mamlaka ya maamuzi kwa yale mambo yanayohusu ofisi kuu ya kanisa na kazi zake za umoja tu na tena mara nyingi ni ushauri tu.
Hata migogoro iliyotokea Meru, Dar es Salaam na Morogoro iliamuliwa na vyombo vya kikatiba vya dayosisi hizo na wala si mkuu wa Kanisa kama ambavyo Askofu Mengele alivyohoji ukimya wake.
Hali hii inatoa mwanya wa uongozi wa KKKT na halmashauri yake kukosa meno ya kuingilia kati pale inapotokea askofu wa dayosisi fulani amehitilafiana na jimbo lake au usharika wake.
Askofu akishindwa kuiongoza vema dayosisi yake, wanaopaswa kumwajibisha ni halmashauri kuu ya dayosisi na mkutano mkuu wa dayosisi husika na si mkuu wa kanisa. Huku ni kukimbia vivuli vyao.
Kwa maana hii, KKKT linapaswa kuitazama upya katiba yake na kuiwekea vifungu vitakavyoiwezesha mamlaka ya juu ya kanisa hilo, kuwa na meno kuingilia migogoro iliyoshindikana ndani ya dayosisi.
Kanisa hili likiendelea na muundo huu, tutaendelea kumbebesha mkuu wa Kanisa lawama ambazo hastahili kubebeshwa, kwa sababu tu askofu fulani ameshindwa kuiongoza vyema dayosisi yake.
Chanzo;Mwananchi

Post a Comment