"Mtanzania kuwa maskini ni ujinga" Mch. Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako'

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu kama ‘Mzee wa Upako’ bado anaamini kuwa Mtanzania kufa masikini ni ujinga na hii ni kutokana na rasilimali zilizopo ndani ya nchi.

Tokeo la picha la mzee wa upako
Mzee wa Upako amesema Tanzania tuna mbuga za wanyama, madini ya Tanzanite, ardhi yenye rutuba hivyo haiwezekani mtu kufa masikini.

“Kufa masikini ni ujinga, halafu ukute ulipata nafasi na fursa mbali mbali huko,“amesema Mzee wa Upako kwenye kipindi cha Maisha Mseto cha Times FM na kusisitiza.

“Tuna mbuga za wanyama , tuna Tanzanite, tuna almasi, tuna ardhi bora, Tanzania ni nchi ya pili katika Afrika kuwa na mifugoo mingi, halafu bado sisi ni masikini? mimi akili haikubali.“amesema Mzee wa Upako na kutoa mfano.

“Kuna nchi moja Singapore wanaendesha nchi yako kwa bandari tu lakini matajiri wanaikimbilia Japan, kwa hiyo mimi siamini Katika umasikini, sisi sio wazima tumerogwa.” amemaliza Mzee wa Upako.


No comments