SIMBA NA YANGA ZAIPAISHA TANZANIA.


 -Kwa mara ya kwanza kwenye historia Tanzania ni nchi pekee ambayo imefanikiwa kupeleka timu 2 kwenye klabu bingwa Afrika (CAF Champion League) timu zetu zimefuzu robo fainali zikiwa ndio timu zilizofunga magoli mengi hatua ya makundi magoli 9 hakuna timu yoyote iliyofunga magoli 9 kwenye hatua ya makundi. 


-Kama nchi tumetengeneza pointi 30 msimu huu ikiwa Simba ametegeneza pointi 15 na Yanga ametegeneza pointi 15 kwa kufuzu robo fainali na kwa sasa tuna pointi 71 nafasi ya sita kwenye association ranking tukiwa tunazidiwa na mataifa 5 makubwa Misri (149), Morocco (138), Algeria (114), Afrika Kusini (101) na Tunisia (87) kwa sasa tuna uhakika wa kupeleka timu 4 kwenye mashindano ya CAF kwa misimu 2 mbele. 


-Pointi 71 zemetegenezwa na timu 3 Simba wametegeneza pointi 39, Yanga Pointi 31 na Namungo pointi 1. Klabu ya Simba kwenye Club ranking ipo nafasi ya 5 sawa na Petro De Luanda ya Angola ikiwa imezidiwa na timu za Al ahly (72), Wydad (69), Esperance (51), na Mamelodi (48) huku Yanga ikiwa nafasi ya 12 kwenye Club ranking ikiwa na pointi 31 na Namungo ipo nafasi ya 69 ikiwa na pointi 1.


-Katika hatua ya robo fainali ambayo itajulikana keshokutwa (March 05) Simba anaweza kukutana na timu zifuatazo Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Ahly ya Misri na Petro de Luanda ya Angola wakati Yanga inaweza kukutana na timu zifuatazo Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Petro de Luanda ya Angola na Asec ya Ivory Coast.


-Iwapo timu zetu zitafanikiwa kufuzu nusu kama nchi tutaongeza pointi 10 na iwapo itafuzu timu moja kama nchi tutaongeza pointi 5 kama nchi na kila Mtanzania anapaswa kuziombea sana Simba na Yanga kwanza kwenye draw wapangwe na timu ambazo wanaweza kuzitoa na kufuzu nusu kwani timu zetu (Simba na Yanga) zitaanzia nyumbani March 29-31 na kumalizia ugenini. 


-Kila la Kheri Simba na Yanga 

-Hongera sana Simba na Yanga 



No comments