Mr Ibu amefariki Dunia
Mchekeshaji na Mwigizaji Legend wa Nollywood Nigeria John Okafor maarufu Mr Ibu, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 62, Vyombo mbalimbali vya Habari Nchini Nigeria vimeripoti.
Ripoti zinasema Mr. Ibu amefariki akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali Jijini Lagos March 02,2024 lakini bado Familia yake haijatoa taarifa rasmi kuhusu kifo cha Staa huyo ambaye alipata umaarufu miaka zaidi ya 20 iliyopita kwenye filamu ya Mr. Ibu iliyompa jina la kisanii alilodumu nalo.
Watu hawakujua kuwa Mr. Ibu anaugua mpaka pale aliposherehekea Birthday yake ya kutimiza miaka 62 October mwaka jana akiwa amelazwa Hospitali ambapo alitumia nafasi hiyo kuomba Watu wamchangie ili alipie bili za Hospitali ambapo Familia yake ilisema alikuwa na tatizo la damu kuganda ndani ya mguu wake na shida nyingine za kiafya ambapo baada ya kufanyiwa upasuaji mara saba mguu wake mmoja ulikatwa mwezi November 2023 ili kuokoa maisha yake.
Baadaye ripoti kubwa ambayo ilihusu Familia ya Mr. Ibu ni pale Watoto wake wawili Daniel Okafar na Mtoto aliyemuasili (adopt) Jasmine Chioma walikamatwa na Polisi kwa kosa la kuingia kwenye simu ya Mr. Ibu bila taarifa yake na kuiba pesa USD 60,700 (Mil. 154.2) ambazo Watu walichanga kwa ajili ya matibabu ya Mr. Ibu .
Itakumbukwa mwaka 2019 Mr. Ibu alilalamika kuwa kuna Ndugu zake wa damu wamewalipa baadhi ya Wafanyakazi wake wa nyumbani ili wampe sumu kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata kwenye kazi zake ambapo baadaye mwezi May 2022 pia Mr. Ibu alilalamika kuwa amepewa sumu kwa mara ya tatu na kusema kuwa amekuwa nusu Mtu na nusu Mfu “Nilishawaona Watu wa upande wa pili wa Dunia lakini Mungu akanirudishia tena uhai wangu, niliwaambia Madaktari pambaneni nipone nikifa Maadui zangu watafurahi“
Post a Comment