Mshambuliaji Prince Dube ametangaza kuondoka Azam FC


 “Ninapoendelea na sura mpya katika kazi yangu ninabeba masomo niliyojifunza wakati nikiwa Azam FC, sapoti niliyopata kutoka kwa mashabiki ilikuwa ya ajabu. Nami nitathamini daima kumbukumbu tulizoweka pamoja.” amesema Dube kupitia barua yake 'thank you' kwa Azam FC


“Nina imani na nguvu na uwezo wa klabu hii, na sina shaka Azam FC itaendelea kufikia mambo makubwa. Nawatakia Azam FC, wachezaji wenzangu makocha na mashabiki mafanikio na furaha. Ahsante kwa safari ya ajabu.”


Ipo hivi ⚽️ 

- Mazungumzo kati ya Azam na Striker wao, Prince Dube yanaendelea ambapo Azam wanahitaji kiasi cha USD 300,000 sawa na Tsh 765M ili kumuachia mchezaji huyo huku Prince Dube akiwa tayari kulipa kiasi cha USD 230,000 sawa na Tsh 586M ili aweze kuondoka kwa Matajiri wa Chamazi.


- Kilichotokea ni Azam kukataa kiasi cha USD 230,000 ambacho Prince Dube alihitaji kulipa na Prince Dube hahitaji kurudi kambi ya Azam kwakuwa anataka kuondoka klabuni hapo, Azam wanasisitiza kuwa bila USD 300,000 hatamuachia Prince Dube.


- Mazungumzo kati ya Azam na Prince Dube yamefikia hatua hiyo na Prince Dube atarudi tena mezani na Azam siku mbili zijazo ili kukamilisha taratibu zote zilizopo za kimkataba ili aondoke Azam.

Hapo awali Dube aliandika barua ya kuvunja mkataba na Club hiyo na kukubaliwa lakini uzito ulikuja kwenye kiasi cha pesa ambacho anatakiwa kukilipa ili kuvunja mkataba ambacho ni USD 300,000 (zaidi ya Tsh. milioni 700) pesa ambazo hadi leo anatoa taarifa hii ya kuaga hajazilipa!


hiyo imekaaje? Embu wataalamu tujuzeni.. Toa maoni yako 🔥 

No comments