Kawa za Tanzania zazinduliwa Japan


 Kampuni ya ITO EN LTD, Kampuni tanzu ya Tully’s Co. Ltd inayomiliki Migahawa maarufu ya Tully’s Coffee, leo tarehe 14 Machi 2024 jijini Tokyo, imezindua aina tatu mpya za Kahawa ya Tanzania, nchini Japan. 


Aina hizo za Kahawa ya Tanzania ni TULLY’s COFFEE BARISTA BLACK KILIMANJARO; TULLY’S COFFEE MY HOME BLACK KILIMANJARO na TULLY’S COFFEE BARISTA ROAST COLD BREW – KILIMANJARO BLEND. 


Kahawa hizo ni kutoka maeneo ya Tarime, mkoani Arusha na mashamba ya GDM yaliyoko Mbozi mkoani Mbeya.


Zoezi hilo la uzinduzi lilifanyika katika Ubalozi wa Tanzania, jijini Tokyo na kuongozwa na Mheshimiwa Baraka Luvanda, Balozi wa Tanzania nchini Japan pamoja na Bw. Osamu Aizawa, Meneja Mkuu wa Kampuni ya ITO EN aliyeambatana na wawakilishi wa kampuni hiyo na Kampuni ya Tully’s Coffee.


Uzinduzi huo ulipambwa na zoezi la uonjaji wa kahawa ya Tanzania iliyozinduliwa ambalo, lilishirikisha wataalam wa kahawa (baristas) wapatao 30 wa maeneo mbalimbali nchini Japan.



Kampuni ya ITO EN Ltd., ni kampuni inayoongoza kwa biashara ya vinywaji nchini Japan ambayo, ni kampuni tanzu ya Tully’s Coffee inayomiliki migahawa ya kahawa takriban 700 nchini Japan na imejipatia umaarufu mkubwa katika biashara ya uuzaji wa kahawa za aina mbalimbali duniani. Kahawa ya Tanzania iliyozinduliwa ni kutoka Mashamba ya kahawa ya GDM (GDM Farms) yaliyoko Mbozi mkoani Mbeya. Hii ni mara ya pili, kwa Kampuni ya Tully’s kuzindua kahawa ya Tanzania katika migahawa yake, uzinduzi kama huu ulifanyika pia mwaka jana mwezi Juni na Agosti, kwa aina ya GDM full washed, GDM natural na Tarime Coffee.


No comments