ARSENAL WAMEFURAHI
✍🏻Aina ya mechi ambayo Physically inachosha sana , maana kasi , nguvu , watu wana sprint sana , pressing , runs za kutosha na ndio maana kuna nyakati fulani uliona kama baadhi ya wachezaji wamechoka sana
✍🏻Hawa wawili Klopp na Pep wakikutana unajua kabisa watafanyaje hivi karibuni wamekuwa hawabadilishi sana mbinu zao
A: LIVERPOOL
✍🏻Wakiwa na mali leo Klopp anajua kabisa kama City bila mpira wanakuwa 4-4-2 na ndio Liverpool wakawa nyuma watatu : Quansah VVD na Gomez huku mbele yao viungo wawili Mac Allister na Endo ... Elliot anaingia ndani kutoka kulia ili kuwa namba 10 wawili yeye na Szobo na Bradley kuwa winga wa kulia ( 3-2-2-3 )
✍🏻Kwanini ? Kwasababu Klopp alikuwa anataka katika kila hatua ya mchezo asiwe na wachezaji pungufu nyuma katikati na mbele ... inasaidia nini ? Inakupa nafasi ya kuishinda pressing ya City , lakini pia timu inasogea juu kwa idadi kubwa ya wachezaji .
✍🏻Bila mpira Liverpool haraka sana wanakuwa 4-1-4-1 , kukabiliana na build up ya Man City ambayo Stones anaongezeka kwenye kiungo lakini pia kufanya pressing haraka sana wakipoteza mpira kuwazuia City wasimpate KDB na Foden kwa haraka .
B : MAN CITY
✍🏻Uwepo wa Stones maana yake unaongeza " control " kwenye kiungo akiwa na Rodri , Silva na KDB kwenye namba 10 wawili nafikiri Liverpool kukabia juu na kufanya distance kuwa ndogo sana baina ya mstari wa ulinzi na mstari wao wa ushambuliaji ( Compact ) uliwazuia City kucheza ndani zaidi bali walienda pembeni zaidi .
✍🏻Pressing ya Man City haikuwa " aggressive " sana yenye nguvu ndio maana Liverpool kupitia Maca na Endo walikuwa wanatoka nyuma na mali kuwalisha watu wa mbele , KDB na Haaland walikosa back up nyuma yao kufunga spaces nyuma yao ndio maana Liverpool walikuwa wanapiga sana pasi za mbele.
NOTE
1: Luis Diaz leo daah kirahisi sana alikuwa anatupia hata kamba mbili peke yake
2: Haaland bila huduma anakuwa abaria uwanjani tu
3: Mac Allister alikishika kiungo haswa utulivu wa hali ya juu
4: Ile kona ya goli Man City imetoka uwanja wa mazoezi 100% 🔥
5: Wataru ENDO daah anakichafua sana , anazuia vizuri , anapiga pasi vizuri , anatunza mali vizuri
Post a Comment