Mo Dewji kaipeleka Yanga robo fainali CAF-CL
Afisa Habari wa Klabu ya Simba SC Ahmed Ally, amegusia juu ya Watani wao Yanga SC kutinga hatua ya Robo fainali Klabu Bingwa Afrika, kwa kusema kuwa Safari ya Yanga Sc katika soka la kimataifa muasisi wake ni Rais wa Heshima wa Simba Sc Mohammed Dewji
“Yanga kufuzu robo fainali wa kupongezwa na wa kushukuriwa ni Rais wa heshima wa Simba SC Mohamed Dewji na wa pili anaepaswa kupongezwa ni Simba SC
“Simba Na Mohamed Dewji tusingekuwa na maono ya kufika kwenye soka la Afrika hakuna klabu ambayo ingefanya wanayofanya hayo leo sababu Mohamed Dewji ndiye aliyefanya timu nyingine ziamke “
“Mohamed Dewji wakati anaanza sera yake ya kuwekeza Simba SC alisema anataka Simba SC ichukue Ubingwa wa Afrika lakini wakati huo vilabu vingine vilikuwa vimelala usingizi wa pono na walikuwa wameridhika kushindana humu kwenye soka la nyumbani”
Ahmed Ally, Afisa Habari na Mawasiliano Simba sports Club
Post a Comment