"Kupata mshambuliaji mzuri sio Rahisi" Ahmed Ally
✍🏾"Katika orodha ya wafungaji 10 Bora kwenye michuano ya AFCON iliyomalizika Nchini Ivory Coast, Tisa kati yao wanatoka ligi za Nje ya Afrika na mmoja anacheza ligi ya Afrika Mabululu kutoka Al Ittihad ya Misri.
✍🏾Kwenye mechi 15 za hatua ya Mtoano za AFCON mechi Tano zilienda hatua ya Penati maana ake ni kwamba Washambuliaji walishindwa kumaliza mechi kwenye dakika 90 .
✍🏾Hii inakupa taswira kuwa Afrika tuna changamoto kwenye eneo la ushambuliaji
✍🏾Al Ahly wamesajili mshambuliaji raia wa Ufaransa aliyekua anacheza timu kubwa Ujerumani Antony Modeste Lakini nae ameshindwa kuonesha makali yake
✍🏾Kocha wa zamani wa Al Ahly Mokthar Mokhtar amesema mchezaji huyo sio Level za Al Ahly
✍🏾Hoja yangu ni kwamba hii ndo nafasi ngumu zaidi kumpata mchezaji Afrika
✍🏾Sisemi kwamba hakuna Washambuliaji wazuri lakini ni wachache kulingana na mahitaji yaliyopo
✍🏾Dirisha dogo la usajili tumesajili Washambuliaji wawili Freddy Michael na Pa Omar Jobe.
✍🏾Freddy mpaka sasa amefunga goli 1 na Asist 1 kwenye mechi 6 alizocheza
✍🏾Jobe amefunga goli 2 kwenye mechi 6
✍🏾Mjadala ni je ni Washambuliaji hao ni wazuri au tumepigwa.
✍🏾Kwa asili ya eneo wanalocheza huwezi kupata majibu ndani ya muda mfupi kama huo.
✍🏾Niwaombe wana Simba wenzangu tuwe wavumilivu, tuwape muda Washambuliaji wetu ili kuwapunguzia presha.
✍🏾Sio rahisi kama tunavyodhani kuwa tunaweza kupata mshambuliaji bora na tishio na akaonesha makali yake ndani ya muda mfupi
CC AHMED ALLY
Vipi semaji la CAF yupo sawa au maoni yako ni yapi?
Post a Comment