π™‹π˜Όπ˜Ύπ™Šπ™ˆπ™€ π˜Ώπ˜Όπ™” ⚽️


 "Kocha Miguel Gamondi baada ya mchezo wa Al Ahly na matokeo tuliyoyapata alikiri kuwa huu utaratibu wa kuita Jina la mchezaji kuelekea michezo yetu ya CAF Champions League unasaidia kuongeza hali ya kupambana na hamasa inaongezeka zaidi, kwa hiyo Kocha wetu Miguel Gamondi amebariki hii Pacome Day na anaifurahia kwa maana umekuwa ni utaratibu unaoleta matokeo chanya."


“Tulianza na mtoko wa Max, Aziz Ki, Bacca na GSM, Mchezo wetu wa awali na CR Belouizidad wengi tulifurahishwa na namna ambavyo timu ilicheza lakini tukahuzunishwa na matokeo. Mchezo huu tunakwenda na agenda kadhaa, kushinda na kulipa deni la magoli matatu. 


“Uongozi na benchi la ufundi tumekubaliana kama taasisi Jumamosi ikawe Pacome Day, ukisema Pacome Day mwisho unamalizia Kitaalamu zaidi, unaweza kupaka rangi kichwani au kwenye ndevu. Kama huwezi kupaka rangi basi unaweza kujichora chochote na wanawake wanaweza kupaka kucha rangi.” 



"Kundi letu liko wazi hakuna mbabe wala mnyonge, yeyote anaweza kufuzu. Sisi Yanga tukimfunga CR Belouizdad πŸ‡©πŸ‡Ώ tutakuwa na asilimia 70% ya kufuzu"


"Sisi hatudeki, kesho Jumanne tutacheza Mchezo wa (FA) dhidi ya Polisi Tanzania Azam Complex na Jumamosi tutakipiga dhidi ya Belouizdad, wale wanaoogopa mechi wanaotaka viporo watuambie kama vipi tuwasaidie tucheze mechi zao halafu points wachukue wao"


©️ Alikamwe

Afisa habari wa Young Africans SC

No comments