Kibabage ni mtu haswa 🔥
Kama mchezaji huwezi kuombea mwenzako aumie, yaani huwezi lakini ikitokea kama ameumia ndio nafasi sasa ya kumuonesha kocha hata mwenzangu akipona haina haja ya kumrudisha kikosi cha kwanza mimi ntaifanya hii kazi : ndicho anachokifanya Nickson Kibabage pale Jangwani
1: Akiwa kiwanjani, Yanga inanufaika na kasi ya akili na mwili wake
2: Jinsi anavyoathiri mechi chanya kwa vitendo vya kiufundi anavyofanya, amekuwa superb
3: Anajua kushambulia space, kutawala eneo la pembeni na kurudi nyuma kusaidiana na walinzi wenzake (Athleticism)
4: Dribbling zake za hatari akitoka nyuma kwenda mbele kuongeza namba nyingi kwenye zone ya mpinzani (Offensive)
Mpira upo kwenye Mahakama yake Nickson Kibabage, hili eneo la kushoto Joyce Lomalisa akulipata kwa mara moja alionesha uwezo : ni wakati wa Kibabage kumuonesha zaidi Master Gamondi kuwa hata kama Lomalisa amepona haina haja ya kumrudisha kikosi cha kwanza mimi naweza kucheza hii nafasi
✍️Nickson Kibabage akiwa compact hana mpira anakuwa kiumbe tofauti, anajituma sana 🔥 : mpaka sasa anatakiwa aboreshe kumwaga maji na kupiga electric pass za mwisho kwa uzuri (Offensive)
Post a Comment