Hali imekuwa tete kwa Kocha EtH pale ManU
Hali inazidi kuwa tete ndani ya Man United , taarifa zinaibuka kutoka Skysports kwamba kocha ETH kuna uwezekano amepoteza imani kwa takribani asilimia 50 ya wachezaji
✍🏻Baadhi ya wachezaji hawana furaha na staili ya uchezaji
✍🏻Wanafikiri wanafanya sana mazoezi , wanakimbia sana mazoezini na hawajui wanakimbia kwa sababu gani
✍🏻Na baadhi ya wachezaji waandamizi wameongea na kocha kutoa maoni yao kwamba wapi wanaamini klabu inapoelekea na nini kifanyike
✍🏻Wametoa maoni yao kuhusu walipotoka katika klabu kubwa kwamba nini walikuwa wanafanya huko
✍🏻Na wengine wametoa maoni yao kwamba hawapendezwi na jinsi Jadon Sancho hali yake ilivyo
RINSE AND REPEAT : Hii hadithi nimeshawahi kuiona huko nyuma dhidi ya makocha wa Man United . Halafu wanaopona ni wachezaji : NYIE hii timu imeoza kabisa . Sijui kocha gani anayejielewa yupo atakuwa tayari kufanya kazi katika hii klabu kwa hali hii ya sasa
ilivyo.
Post a Comment