𝗟𝗨𝗜𝗦 𝗠𝗜𝗤𝗨𝗜𝗦𝗢𝗡𝗘 𝗡𝗜 𝗠𝗭𝗜𝗚𝗢 𝗞𝗪𝗔 𝗞𝗟𝗔𝗕𝗨

"Kuna Jose Luis Miquissone. Sijui kimemtokea nini. Zamani katika mechi kama hi, Miquissone alitazamiwa kuwa mtu wa kuiteketeza Galaxy. Leo anaingia uwanjani dakika ya 70 na bado

hakuna anachofanya. Alipokuja mwanzoni ilitajwa kwamba alikuwa ameongezeka kilo katika mwili wake.Miquissone wa sasa amerudi kuwa na umbo lilelile, lakini anashindwa hata kutuliza mpira uwanjani

achilia mbali kukokota.


Imekuwa, ghafla sana na sasa tunajiuliza kama kweli ataweza kurudisha makali yake yaliyowahi kuifanya Al Ahly kutoa kiasi kikubwa cha pesa kupata huduma zake miaka michache iliyopita. Simba walilia arudi lakini hadi sasa hawaamini wanachokiona. Kama

uongozi utaamua kuachana naye mwishoni mwa msimu sidhani kama kuna Mwanasimba ambaye atapigwa na butwaa.



Amekuwa miongoni mwa wageni mizigo katika klabu hii ambayo ilimtambulisha zaidi barani Afrika. Naanza pia kupatwa na wasiwasi na Jean Baleke. Ni kweli anaibeba Simba kwa kutupia mabao, lakini nje ya mabao hana mchango mkubwa uwanjani. Inabidi abadilike kama kweli anataka kuibeba Simba. Asisubiri mabao ya kugusa tu mpira uende wavuni." -

Mchambuzi Edo Kumwembe.

No comments