Simba na Yanga; Jengeni viwanja vyenu, acheni kulalamika tu


 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema Uwanja wa Benjamin Mkapa utatumika kwa baadhi ya michezo kuchezwa kiwanjani hapo na michezo mingine itachezwa katika viwanja vingine.


Rais Karia amesema uwanja huo utatumika kwa ajili ya michezo ya kimataifa kwa Simba SC na Yanga SC, Taifa Stars na mechi ya Watani wa Jadi.


“ Miundombinu ni jambo ambalo lilikuwa na changamoto sana, sasa hivi viwanja mmeona vinapendeza lakini uwanja wa Taifa ni uwanja wa Serikali. Sisi tunachoangalia ni kuhakikisha uwanja hatuuzidishii matumizi. 


“ Ikiwezekana ligi zetu ichezwe mechi ya Simba SC na Yanga SC tu, kuhusu ligi mechi zinazoihusu Simba SC au Yanga SC zitachezwa sehemu nyingine, ila wanapocheza wao wenyewe sawa na hata timu ya Taifa tunataka tuangalie sehemu nyingine ya kucheza ili uwanja upumue “ alisema Karia.



Rais huyo amesema wana mipango ya kuufanya uwanja huo udumu kwa muda mrefu katika ubora.


Pata Burudani ya kuangalia Tamthilia na mechi Live na BURE kupitia App yetu ya Binago TV, Bofya hapa ku download 👇🏽

Download Binago TV

No comments