Robertinho 𝗔𝗜𝗦𝗛𝗔𝗨𝗥𝗜 𝗬𝗔𝗡𝗚𝗔
Aliyekuwa kocha wa Simba SC, Robertinho ameishauri klabu ya Yanga kwa njia ya simu akiwa njiani Kuelekea Saudi Arabia 🇸🇦 kwenye mapumziko.
"Yanga wana timu nzuri inayoweza kuimaliza Al-Ahly ila kwa kutumia mfumo wa (4-2-3-1) wakiwa hawana mpira, lakini wanaposhambulia wanaweza kubadilika na kutumia (4-3-3) ili kurahisisha mashambulizi"
"Al-Ahly wanacheza tofauti wanapokuwa nyumbani na ugenini. Kwa kuwa Yanga ataanzia nyumbani, ndiyo wanahitaji kucheza hii mechi kwa kuhitaji matokeo mazuri lakini wanatakiwa kuwa makini kwani wapinzani wao wanapenda sana kucheza soka la kushambulia"
"Kama Yanga watatumia mfumo wa (4-3-3) wakati wa kushambulia utawafanya kuwa na idadi nzuri kule mbele katika mashammbulizi yao ambapo itawapa wakati mgumu mabeki wa Al-Ahly ambao hawana utulivu sana"
"Al-Ahly hawana kasi sana ya kukimbia kurudi nyuma kujilinda, hili lazima Yanga walitumie kwa kucheza mpira wa kasi ili wafike langoni kwao kuwapa presha mabeki wao"
"Yanga ina wachezaji bora, ila ina wachezaji (3) wenye ubora zaidi, Aziz Ki, Pacome, Max. Kama wakiamka vizuri siku ya Mchezo wanaweza kuwa hatari katika lango la Al-Ahly"
©️ Robertinho 🇧🇷
Interview — MwanaSpoti
Post a Comment