KOCHA WA ASEC: NIMEISOMA SIMBA, HAWACHOMOKI
Kocha wa ASEC Mimosas amesema ameingalia mechi ya Simba 1 - 5 Yanga na kupitia mechi hiyo itamsaidia kuwakabili Simba November 25. Pia amewataja wachezaji wa Young Afticans SC.
"Nimewaona wote wachezaji wangu wa zamani, lakini nimevutiwa sana na Pacome Zouzoua, nimekuwa namfatilia sana tangu amekuja Tanzania nafikiri kiwango alichokionesha juzi ndio ameanza kucheza kwa ubora wake ninaoujua"
"Lakini pia nimewatazama Simba SC ambao nitakutana nao kwenye hatua ya makundi. Kupitia mechi hiyo na zingine zitatusaidia Kuelekea mchezo ujao"
"Ukiacha goli lake la penati, alitakiwa kufunga zaidi kama angekuwa na utulivu, alipata nafasi za mapema lakini hakuwa ametanguliza utulivu. Niliwahi kuwaambia, huyo Pacome ni mchezaji mkubwa sana"
"Kuhusu Yao, iwapo Yanga watakuwa na washambuliaji bora watafunga sana kupitia krosi zake"
©️ Julien Chevalier 🇫🇷

Post a Comment