𝗗𝗜𝗘𝗡𝗚 𝗞𝗨𝗛𝗨𝗦𝗨 𝗬𝗔𝗡𝗚𝗔
Kiungo tegemeo wa klabu ya Al-Ahly, Aliou Dieng 🇲🇱 amefunguka mengi kuhusu Yanga.
"Ni kweli tumepata fursa kuzitazama video za Yanga SC haswa kwenye mechi ya mwisho dhidi ya CR Belouizdad 🇩🇿 lakini tumegundua kuna mabadiliko makubwa kiuchezaji kwa Yanga, licha ya kupoteza lakini wanacheza soka la kuonana sana"
"Tunajua mchezo utakuwa mgumu, hasa kinachotuumiza kichwa ni kukosa matokeo mazuri kila tunapocheza Nchini Tanzania, tutajitahidi kuona jinsi gani tunapata matokeo bora katika ardhi ngumu ya Tanzania"
"Tulipokuja Tanzania mara ya mwisho kucheza na Simba tuliona kwamba ni mchezo ambao tuliostahili kushinda kwa jinsi tulivyoanza mechi lakini baadae tukafanya makosa ya kuruhusu mabao (2) ya haraka"
"Tunakuja tukijua kwamba tunakwenda kucheza uwanja mgumu kwa sasa kwetu, tunataka kuhakikisha kwamba tunabadilisha haya matokeo ingawa tunajua tunakwenda kukutana na timu nyingine ngumu"
"Naifahamu Yanga, wanawachezaji bora, nawajua baadhi ya wachezaji wa Yanga, nimekuwa nikiifatilia Yanga kupitia kwa Djigui Diarra 🇲🇱, kuna taarifa nzuri kuhusu wao, ndani yake nimekuwa naona wana timu bora, wanafanya vizuri wametoka kucheza fainali (CAF), wachezaji wengi ni wazuri hii itafanya mechi yetu na wao kuwa ngumu"
"Ukiangalia, Djigui Diarra ni kipa wa timu yetu ya Taifa (Mali 🇲🇱) ni kipa mzuri na mkubwa, wapo wachezaji wengine lakini hii kucheza fainali ya (CAF-CC) inatosha kuonesha ni timu nzuri, tunawaheshimu lakini tutapambana nao kutafuta alama tatu"
©️ Aliou Dieng
Interview — Mwanaspoti
.
.
Al-Ahly wanatarajiwa kuwasili usiku wa leo wakiwa na kila kitu hadi mpishi.
Post a Comment