Tuzo za Ballon d'or, Messi Mbabe ⚽️
... 🚨 Jude Bellingham (20) ameshinda tuzo ya mchezaji bora kijana U21 wa Dunia Kopa Trophy kwenye tuzo za Ballon d'or 2023.
Amewashinda hawa wafuatao :
◉ Jude Bellingham 🏴 — 🏆
◉ Jamal Musiala 🇩🇪 — (2nd)
◉ Pedri 🇪🇸 — (3rd)
◉ Eduardo Camavinga 🇫🇷 — (4th)
◉ Gavi 🇪🇸 — (5th)
◉ Xavi Simons 🇳🇱 — (6th)
◉ Alejandro Baldé 🇪🇸 — (7th)
◉ António Silva 🇵🇹 — (8th)
◉ Rasmus Højlund 🇳🇴 — (9th)
Amekuwa Muingereza wa kwanza kuchukua tuzo hii baada ya
◎ 2018 — Kylian Mbappé
◎ 2019 — Matthijs de Ligt
◎ 2021 — Pedri
◎ 2022 — Gavi
◉ 2023 — Jude Bellingham
... 🚨 | Vinicius Jnr ameshinda tuzo ya Utu na Ubinadamu, Socrates Award kwenye tuzo za Ballon d'or kutokana na kupambana na Ubaguzi wa rangi michezoni na kujitoa kusaidia watu wasiojiweza.
Mnamo 2022, uwekezaji wa Vinicius ulifikia euro 335,000, ulizidi euro milioni 1 mnamo 2023, na utafikia euro milioni 2.5 mnamo 2024.
Itakumbukwa tuzo hii ilichukuliwa na Sadio Mane mnamo 2022 kwa kujitolea kwake kwa jamii ambapo alijitolea katika ujenzi wa hospitali katika kijiji chake cha utotoni huko Senegal sambamba na kusaidia timu za mpira wa miguu za vijana, haswa kwa wasichana, ili kuwapa fursa sawa ya michezo.
🚨 Golikipa wa Argentina, Emiliano Martinez 🇦🇷 aneshinda tuzo ya Golikipa bora wa Dunia 'THE 2023 YACHINE TROPHY' kwenye tuzo za Ballon d'or 2023 Nchini France 🇫🇷
🚨 | Erling Haaland ameshinda tuzo ya mshambuliaji bora wa Dunia wa mwaka 'Gerd Muller Award' kwenye tuzo za Ballon d'or.
◉ Games — 53
◉ Goals scored — 52 🔥
Klabu ya Manchester city imechaguliwa kuwa klabu bora ya mwaka Duniani 2023.
🚨 RASMI ⚽️ Kiungo wa Barcelona Women Aitana Bonmati ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Kike wa Dunia wa mwaka 2023, Ballon Dior. 🏆🇪🇸
Tazama Mechi LIVE, Tamthilia na magazeti kila siku kupitia App yetu ya Binago TV, Bofya hapa ku download 👇🏽
https://m.apkpure.com/binago-tv/binago.aplicyzk
Post a Comment