SAFARI NGUMU YA ZINEDINE ZAYID

.

Wakati Nasikiliza Mistari Ya Farid Kubanda kwenye ngoma ya mafaniko pale anaposema "Ukijituma Na Neema Inakaribia Nyuma Waliogive Up Mapema Wangekaza Wangefikia" hii ikanifanya nimkumbuke ZINEDINE ZAYID ZIDANE moja Footballer Icon ambaye Ameacha alama isiyofutika kwenye mioyo ya wapendasoka Duniani na kuona kama tunamdai vile, miguu iliyojaaliwa uwezo wa ajabu wa kufanya mpira anachotaka kama angezaliwa kwetu Brazil tungemuita Zidaninho, nguvu, akili ,maono ya ajabu, control za ajabu, skills za ajabu zilifanya kuacha midomo ya watu wazi, pale anapokuwa uwanjani unahisi mechi imeisha kabla ya kuanza hakika alibarikiwa vitu vingi kwenye miguu hii ilikua ni neema na baraka za Mwenyezi Mungu kwenye miguu ya Zidane miguu iliyobarikiwa Nuru, Nguvu za Duma na akili kama za Terence Tao.


Maestro alizaliwa jijini Ufaransa mwaka 1972 katika jiji la La Castellane, Marseille, Licha ya harakati ngumu za kimaisha za mzeee wake ISMAIL hazikufamfanya kukataa tamaa na mbaya zaidi mama yake alikuwa mama wa nyumbani hakuwa na harakati yeyote ya Kufanya ili kuendeleza familia ya watoto watano majukumu yote yalibaki kwa mzee Ismail, mitaa ambayo alikulia Zidane haina tofauti na mitaa aliyotokea CARLOS TEVEZ kule Fuerte Apache nchini Argentina mitaa hii nayo ilikua na matukio ya Usela mwingi sana uhalifu, ukosefu wa ajira na viwango vya watu kujiua vilikuwa vinongezeka siku baada ya siku haikua mitaa salama kwa mtoto kuishi na ni moja ya kitongoji kinachoongoza kwa wahamiaji na kama unavyojua palipo na Manigga basi Gun iko pembeni muda wowote kinanuka.


Kwa ugumu wa maisha ukamfanya kijana Zizou kutafuta njia sahihi ya kumaliza umaskini katika familia yake na ndipo akajiunga na klabu ya US Saint-Henri mwaka 1981, baada ya kujiunga na klabu hii hakudumu kutokana na kufanyiwa vitendo vya ubaguzi na kuongea maneno mabaya juu yake Walimuita mtoto wa "GHETTO", akaondoka akajiunga na klabu ya SO Septèmes-les-Vallons, ambapo alitumikia mwaka 1983 hadi 1986 na kutimkia zake kwenye klabu ya Cannes kwenye msimu wa 1990-91 Zidane alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Cannes alionyesha ujuzi wa kipaji chake Cha ajabu na kuwasaidia kumaliza nafasi ya nne kwenye Ligue 1.


Haikuishia hapo kwa kijana wa Ghetto akafanya makubwa kwenye klabu ya Bordeaux na ndipo matamanio ya kutaka kutoka ufaransa yaliongezeka pale aliposhinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa 1995-96.


Ofa zikamwagika kwa kijana wa Ghetto ofa kutoka Uingereza pamoja na Italia lakini Mfaransa huyo aliamua kuungana na Black and white licha ya kupokea ofa nyingi kutoka klabu mbalimbali za Ulaya, Newcastle moja ya klabu iliyokuwa ikigombania saini yake lakini zote alizikataa na kipindi hiko Newcastle ilikua ya moto sana.


Baada ya kusajiliwa Juventus alifanikiwa kushinda Serie A mara mbili mfululizo pia walitinga fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa misimu yote miwili, lakini wakaishia kupoteza mara zote mbili kwa wababe wa Ujerumani Borussia Dortmund na vinara wa Hispania Real Madrid Ingawa alikuwa tayari ameshinda kila kitu kwenye ngazi ya taifa kwa kipindi chake akiwa Juve, alikua na kiu sana ya kushinda Uefa champions league, Alijiunga na Los Blancos kwa rekodi ya dunia kwa kipindi hicho.


Zinedine Zidane alikubali kujiunga na wababe wa Hispania kwa ada kiasi cha €77.5 M mnamo 2001, rekodi ambayo haikuvunjwa kwa miaka 8, Matarajio yalikuwa makubwa na yakiongezeka kwa Zizou alipoungana na wachezaji bora wa dunia kama vile Raul, David Beckham, Luis Figo, na Roberto Carlos na katika msimu wake huo huo wa kwanza alifanikiwa kushinda Champions League huku akifunga bao la kumbukumbu lililowapa madrid ubingwa mbele Bayer Leverksen, katika fainali ambayo inabaki kuwa moja fainali bora katika maisha yake, Zidane aliiwezesha Real Madrid kushinda taji la Hispania La Liga msimu uliofuata alinyakua tuzo ya Ballon d'Or na tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia wa FIFA, Dunia bado inamtafuta ZINEDINE ZAYID bado haijampata yuko wapi mtu kama wa hivi na kama yupo kwanini kajificha wakati dunia inataka ladha ya soka, Zidane aliweza kuwa shujaa wa taifa la ufaransa baada ya kuisaidia kufikia ndoto iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu kwa kutinga fainali ya Kombe la Dunia na kuwashinda mabingwa watetezi Brazil mwaka 1998 na kushinda Euro mwaka 2000 Zidane aliamua kutundika daruga mwaka 2006, muda mfupi baada ya kutimiza miaka 34, huku fainali ya Kombe la Dunia 2006 ikiwa ni mchezo wake wa mwisho.


Namalizia Kusema Watu Wagumu Watapita Ila Nyakati Ngumu Hazita Sahaulika.


CREDITED: Michezo live

No comments