Mwili Mdogo wa Ngassa hauna nafasi Ulaya
"Mwili Mdogo wa Ngassa hauna nafasi Ulaya"⚽
⚽ Mwezi Aprili mwaka 2009 Yussuph Bakhresa alimpeleka Ngassa kufanya majaribio katika klabu ya West Ham united ya England na ilielezwa kuwa kocha wa West Ham united kwa Kipindi hicho Gianfranco Zola alivutiwa sana na kiwango cha Nyota huyo Kutokea Tanzania .
⚽ Lakini shida ikawa ni kwenye Mwili wa Nyota huyo ilielezwa kuwa west Ham walimkataa Ngassa kisa ana mwili mdogo na akaambiwa arudi Afrika kuja kujenga Mwili wake Kwanza japo ndio ilikuwa imeisha .
⚽ Lakini kama ipo ipo tu mwezi july mwaka 2011 Ngassa akafuzu majaribio mengine safari hii ilikuwa Marekani katika klabu ya Seattle Sounders ambayo ilikuwa inashiriki ligi kuu ya Marekani .
⚽ kama uliwahi kusikia Ngassa alicheza na Manchester united ya kina Rio Frednand basi ilikuwa ni sehemu ya majaribio yake katika klabu hiyo ya Seattle Sounders ambapo alipewa dakika 14 za kucheza katika mchezo ambao klabu hiyo ilicheza na Manchester united
⚽ Sasa wakati Ngassa anafanya majaribio kulikuwa na Mchezaji Mwingine ambaye pia alikuwa anafanya majaribio na alikuwani mchezaji kutoea jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na inaelezwa kuwa Kocha wa Timu hiyo Sigi Schmid alivutiwa zaidi na mkongo huyo
⚽ Ngassa akapewa ahadi tena akaambiwa kama itatokea Nafasi nyingi basi ataitwa ahadi ya mchongo ambayo haijatimia mpaka leo .
⚽ Ulaya sio mchezo Ngassa ambaye ni moja kati ya kiungo mshambuliaji hatari kuwahi kucheza katika ligi yetu alipoteza Nafasi mbili za kucheza Ulaya kisa mwili wake ulikuwa mdogo
Post a Comment