Bernard Morrison kutua Yanga SC

"Sasa rasmi Morrison ni mali ya Young Africans SC,, Taarifa za kuaminika ni kuwa, mchezaji Bernard Morrison yuko kwenye hatua za mwisho kumalizana na Yanga SC"

"Morrison alitakiwa kusafiri wiki hii kwenda kwao Ghana 🇬🇭, na uongozi wa Simba ulishafanya taratibu zote za kumkatia tiketi"

"Lakini kwa hali isiyotarajiwa, viongozi wa Simba wakimpigia simu kumuuliza kuhusu safari yake hapokei simu wala hajibu msg"

"Katika hali ya kushangaza zaidi afisa wa Simba SC aliyekuwa akimpigia simu Morrison alipokea mtu aliyejitambulisha kwa jina la HAJI, akimuonya kuwa aache kumpigia simu Morrison"

"Afisa wa Simba aliendelea kupiga simu ya Morrison, akapigiwa tena na mtu yuleyule na kumueleza ujumbe uleule kuwa aache kumsumbua Morrison"

"Imefahamika kuwa Morrison atasafirishwa na Yanga kwenda Mwanza kushuhudia mchezo wa nusu fainali ya Azam sports"

🔍 Jemedari Said mchambuzi

No comments