𝗧𝗘𝗧𝗘𝗦𝗜 𝗭𝗔 𝗦𝗢𝗞𝗔 𝗨𝗟𝗔𝗬𝗔 𝗝𝗨𝗠𝗔𝗡𝗡𝗘 24/05/2022


➪Erik ten Hag ameweka bayana kwamba anataka mshambuliaji Cristiano Ronaldo, 37, kusalia Manchester United kwa msimu mwingine. (Metro)

➪Tottenham watamenyana na wapinzani wao Arsenal katika usajili wa mshambuliaji Gabriel Jesus, 25, kutoka Manchester City. (Telegraph)

➪Real Madrid inataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, 27, baada ya kumkosa mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 23. (Star)

➪Spurs wanakaribia kufikia mkataba wa uhamisho wa bila malipo wa kipa wa Southampton Fraser Forster, 34. (Mail)

➪Kiungo wa Leicester Youri Tielemans, 25, ni mmoja wa wachezaji wanaolengwa na mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta msimu huu wa joto. (Telegraph)

➪The Gunners watajaribu kuwauza karibu wachezaji saba wa kikosi cha kwanza msimu huu wa joto akiwemo beki Hector Bellerin, 27, na kipa Bernd Leno, 30. (Sun)

➪Juventus wamepiga hatua katika juhudi za kumsajili mlinzi wa Arsenal Gabriel, 24. (Mirror)

➪Leeds wako tayari kumsajili kiungo wa kati wa Kimataifa wa Marekani Brenden Aaronson, 21, kutoka Red Bull Salzburg kwamkataba wa £23m . (Times)

➪Mkufunzi wa Napoli Luciano Spalletti amesisitiza kuwa haiwezi kumuuza mchezaj wa kimataifa wa senegal anayenyatiwa na Chelsea Kalidou Koulibaly,30. (Star)

➪Patrick Vieira anasema Crystal Palace ingependelea kiungo wa kati wa England wa miaka 22-Conor Gallagher arejee Selhurst Park kutoka Chelsea msimu ujao. (Star)

No comments