Hii nchi naona uhuru umepitiliza !! 😆
Yaani bajeti ya Tsh Bilioni (2) na nusu kwa ajili ya usajili wa Wachezaji wapya (5) ni ndogo sana ?!! 😮
.
.
Hakuna klabu East Africa ambayo imewahi kutumia Tsh Bilioni (2) na nusu kununua Wachezaji (5), hii nguvu ya kusema Bilioni (2.5) ni ndogo sana hawa WACHAMBUZI wanaitoa wapi ?!!
.
.
Klabu inayotolewa mfano East Africa Simba sc na inayofanya vizuri kimataifa, usajili wao mkubwa zaidi uliogharimu pesa nyingi ni wa Sadio Kanoute kutoka Al Ahly Benghazi 🇱🇾,, Kanoute alisajiliwa kwa Tsh Milioni (347)
.
.
Katika bajeti hiyo ya Tsh Bilioni (2) na nusu unanunua Wachezaji zaidi ya (9) wenye thamani ya Kanoute, yaani Milioni (347) kila mmoja na chenji inabaki.
.
.
Tsh Bilioni (2) na nusu kwa idadi ya Wachezaji wapya (5) wakubwa Africa wanaohitajika na Yanga, ina maana kila mchezaji atanunuliwa kwa Tsh Milioni 500.
.
.
Mchezaji wa Tsh 500 Milioni Africa ni mchezaji wa kiwango cha juu sana. Kuhoji eti Bilioni (2) na nusu ni ndogo sana kwa usajili wa wachezaji (5) wapya ni MATUSI.
0 Comments