Mayale ni Cristiano Ronaldo wa Bongo

Ameandika Samuel Samuel.

NAKATAA KWA NGUVU ZOTE MAYELE SI DARAJA LA KAWAIDA 

Nimeuona mjadala mtandaoni ambao kwa kiasi kikubwa umenishitua na kuniogopesha . “ Mayele ni mshambuliaji wa kawaida, tena kawaida sana “ 

Mwenye mjadala amekuja na hoja za kisomi kabisa kwa maana ya ‘ namba za ulinganifu kutetea hoja ‘ . Well and good.

Lakini kwenye mijadala ya uzuri, ubora , ubaya au ulinganifu wowote ule ambao upo practically oriented, hutakiwi kuangalia variable moja tu ya rekodi ya namba . Lazima ujiongeze na vitu vingine ili uwe fair .
Yanga hii ya FISTON MAYELE mwenye goli 11 ligi kuu Tanzania bara msimu ukiwa unaendelea baada ya timu yake kucheza mechi 20, isikufanye kumchukulia poa huyu mwamba kwa kumlinganisha tu na wenzake huko nyuma . 

Yanga hii ina tatizo kubwa eneo la kiungo hususani viungo wa pembeni kitu ambacho sometimes kinamfanya Mayele kushuka chini kucheza deep .

Kila uchao Nabi bado haridhishwi na uchezaji wa washambuliaji wake wa pembeni au viungo wa pembeni . Hawatengenezi nafasi nyingi za kufunga , mipira mingi hupotea kwao. Alianza na Moloko akahitaji wasaidizi na kuletewa Nkane, Ngushi na Ushindi ambao  bado utaomba Moloko asiumie .

Kule kushoto tangu aumie Yacouba bado tia maji licha ya mzee wa kazi Saido kupambana vilivyo lakini utaona ni aina ya wachezaji ambaye anapenda kuwa huru pale mbele.

Kati ukiwakosa Aucho na Feisal timu ina struggle ku-maintain umbo . JE UNAIKUMBUKA KAMPA KAMPA TENA ? Mayele angekutana na wale watu ingekuwaje ? 

Mjadala umerudi nyuma hadi miaka ya 90 na mwanzoni mwa miaka ya 2000. Jamani zile dhahabu uwanjani bado zipo? Sekilojo, Lunyamila, Kizota, Akida , Shaaban Ramadhan, kwanini Mmachinga asitakate pale mbele. 

Fullbacks kama Fuso unakosaje kumwagiwa maji ya hatari unywe? 

Nabi anakataa kabisa kumuona Makambo garasa na kuwalaumu wapishi wa pembeni kujua namna ya kumchezesha mtu kama yeye. Mnamkumbuka Ajibu na Makambo wake kwa Zahera? 

Binafsi namuona Mayele ni BULL STRIKER. Mpira umebadilika sana na anapambana sana kuipa heshima Yanga na ligi yetu . Ikumbukwe kule DRC alimaliza mtu wa pili nyuma ya mfugaji bora msimu wa 2020-21 akiwa na goli 14.

Mjadala utazame pia aina ya ligi, mabadiliko katika mbinu na ufundi, aina ya wachezaji wanaomzunguka mchezaji fulani. Sense of vulnerability itazamwe pia . Marekani huzoa medali nyingi za dhahabu katika michezo ya Olympic kwakuwa huwa na wachezaji wengi wazuri kila idara na kila mchezo . Mayele ni mmoja tu na anapambana . Naamini ndio kiumbe anaekumbukwa sana katika dua za wanajangwani. 

Timu ikiwa na key players wengi nafasi moja pia uwezekano wa ubora kulindwa huwa mkubwa . Kumbuka kikosi hiki;
Makipa:Ali Mustafa,Deo Munishi na Yusuph Abdul.Mabeki wa kulia ni:Mbuyu Twite na Juma Abdul huku kushoto wakiwa ni Oscar Joshua na David Luhende,mabeki wa kati ni Nadir Haroub,Kelvin Yondani na Rajabu Zahir.
Viungo ni Athumani Idd chuji,Frank Domayo,Haruna Niyonzima,Somon Msuva,Salum Telela,Reliants Lusajo,Nizar Khalfan,Washambiliaji ni Didier Kavumbagu,Jerryson Tegete,Mrisho Ngasa,Shabani Kondo na Huseni Javu(22players).



No comments