Hawa hapa vinara wa mabao ligi za east Africa

WAKAWAIDA SANA !
Vinara wa mabao east Africa !

🇹🇿 🎱 19 ⚽ 11 = Fiston Mayele (Yanga)
🇺🇬 🎱 25 ⚽ 11 = Mukwala steven (URA)
🇰🇪 🎱 25 ⚽ 10 = Miheso (Polisi fc) 
🇨🇩 🎱 23 ⚽ 09 = Makabi Lilepo (AS Vita)
🇷🇼 🎱 22 ⚽ 09 = Bigirimana (Kiyovu)
.
.
Mshambuliaji wa klabu ya Young Africans Fiston Mayele 🇨🇩 (28) anaongoza kwa uwiiano mzuri wa mabao na idadi ya mechi alizocheza East Africa.
.
.
Mayele amecheza michezo (19) huku akihusika kwenye mabao (14) katika ligi kuu Tanzania bara... Mayele ni miongoni mwa Wachezaji wachache wanaoongoza kwa mabao mengi bila kuwa na bao lolote lile alilofunga kwa mkwaju wa penati.
.
.
Mechi dhidi ya Geita gold na dhidi ya Mbeya city magoli yake halali yalikataliwa, inamaana angekuwa na mabao zaidi ya (13) so far.
.
.
Mayele angekuwa anapiga penati kama baadhi ya vinara wengine wa mabao huenda angekuwa na mabao zaidi ya (15).
.
.
WAKAWAIDA SANA !!! Mabadiliko ya soka Duniani ni makubwa sana, inashangazaa na inasikitisha kwa baadhi yetu kujitia upofu na uendawazimu wa kutojua hilo. Hawajui kuwa soka la sasa limebadilika na ushindani hasa katika ligi yetu umekuwa ? 

Nadhani ni kiburi tu.
.
.
Zamani ilikuwa nadra kuona klabu kama Coastal Union inamiliki mchezaji kutoka Nigeria 🇳🇬, klabu kama Namungo inamiliki Wachezaji kutoka Dr Congo 🇨🇩, Burundi 🇧🇮 nk... Lakini kwa sasa ni jambo la kawaida.
.
.
Huwezi kufananisha ligi ya zamani na sasa, ligi ya sasa inaushindani zaidi, tafakari,, timu ya mwisho kwenye msimamo itakayoshuka daraja itapewa Bonus ya pesa,, Timu bingwa atapata 500 Milioni, wa pili 250 Milioni, wa tatu 200 Milioni hivyo hadi anayeshika mkia.
.
.Nakuhakikishia, hao Wachezaji waliokuwa wanafikisha magoli (25) zamani, ukiwaleta katika ligi ya sasa wakijitahidi sana wataambulia magoli (15) au (16). Ilikuwa ni kawaida kwenye ligi yetu timu kufungwa mabao (7) (6) (5) lakini msimu huu hakuna timu ilitofungwa bao hata (5) tu ligi kuu.
.
.
Msimu uliopita (2020-21) akiwa Dr Congo 🇨🇩 Fiston Mayele ndiye aliyeipa ubingwa As Vita kwa kufunga mabao muhimu (13) akiwa kinara wa mabao AS Vita na kinara wa pili kwenye ligi ya Dr Congo nyuma ya Jean Baleke wa Tp Mazembe aliyefunga mabao (14) kwenye ligi kuu ya Dr Congo Linafoot.
.
.
Msimu wa (2019 - 20) alifunga mabao (12) Dr Congo, nazungumzia Dr Congo sio ligi ya mbuzi imagine halafu unamuita MCHEZAJI WA KAWAIDA SANA.
.
.
MCHEZAJI WA KAWAIDA SANA amefunga mabao (4) na kutoa assists (3) katika michezo (13) (CAF) CHAMPIONS LEAGUE,, Yaani michezo (13) klabu bingwa Africa amehusika katika mabao (7).
.
.
Unamuhukumu vipi Mayele kwa kufunga mabao (11) ilihali bado ana michezo (11) mkononi !!! Inafikirisha sana, wanaoanzisha hoja hizi mfu wanalengo gani ?!! Bila shaka hii ni DALILI YA UCHAWI.

No comments