AMKA NA BWANA LEO 24/04/2022
KUWA NA USHIRIKA NA YESU KUPITIA NENO
Na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiliza imani yetu. Waebrania 12:1, 2.
⏯ Hakuna mwanamme, mwanamke, au kijana anayeweza kufikia ukamilifu wa Kikristo na kupuuzia kujifunza Neno la Mungu. Kwa kujifunza Neno la Mungu kwa uangalifu na kwa karibu tutatii amri ya Kristo, "Mwayachunguza Maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia." Uchunguzi huu humwezesha mwanafunzi kuangalia kwa karibu mfano wa Mungu, kwa kuwa yanamshuhudia Kristo. Sampuli inapaswa kukaguliwa mara nyingi na kwa karibu ili kuiiga.
⏯ Wakati wanadamu wanakuwa na uzoefu wa historia ya Mkombozi, wanagundua mapungufu ya tabia ndani yao wenyewe; kutofanana kwao na Kristo ni kukubwa mno kiasi kwamba wanaona kuwa hawawezi kuwa wafuasi bila ya mabadiliko makubwa katika maisha yao. Bado wanajifunza, kwa shauku kuwa kama mfano wao mkubwa; wanapata mtizamo, roho, ya Mwalimu wao Mkuu; kwa kumtazama wanabadilishwa. "Tukimtazama Yesu mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza Imani yetu." Sio kwa kuangalia mbali kutoka Kwake, na kwa kutomtazama, kwamba tunaiga maisha ya Yesu; bali katika kukaa na kuzungumza kuhusu Yeye, na kutafuta kuendea Mfano bora kwa njia ya juhudi ya bidii, kupitia imani na upendo.
⏯ Usikivu ukiwa umeelekezwa kwa Kristo, sura Yake, safi na isiyo na doa, kutunzwa ndani ya moyo kama "Mashuhuri miongoni mwa makumi elfu na mmoja wa kupendeza kabisa." Hata bila kujua tunaiga ile ambayo tunaijua. Kwa kuwa na ufahamu wa Kristo, wa Neno Lake, Tabia Yake, masomo Yake ya maagizo, kwa kukopa uzuri wa tabia ambayo tumeijifunza kwa karibu, tunajazwa na roho ya Bwana ambayo tumekuwa tukiitamani sana....
🔘 Neno la Mungu, likizungumzwa moyoni, lina nguvu ya uhuishaji, na wale watakao jifanyia kisingizio cha kupuuza kupata uzoefu wake watapuuzia madai ya Mungu katika maeneo mengi. Tabia itaharibiwa, maneno na matendo lawama kwa ukweli.
MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA
Post a Comment