AMKA NA BWANA LEO 12/04/2022

KESHA LA ASUBUHI 

JUMANNE, APRILI 12 2022

CHUNGUZA KWA BIDII KILA IMANI 

Nikageuka, na moyo wangu ulikazwa katika kujua na kupeleleza, na kuitafuta hekima, na maana ya mambo yaliyoko; ili nifahamu ya kuwa uovu ni upumbavu, na upumbavu ni wazimu. Mhubiri 7:25.

▶️ Nimeoneshwa kuwa wengi wanaokiri kuwa na ufahamu wa ukweli wa sasa hawajui kile wanachokiamini. Hawaelewi ushahidi wa imani yao. Hawana utambuzi wa thamani ya kazi ya wakati huu. Wakati wa majaribio utakapokuja, kuna watu wanaohubiri kwa wengine sasa ambao wataona, katika kuchunguza nafasi walizo nazo, kwamba kuna mambo mengi ambayo kwayo hawawezi kutoa sababu Hawakuujua ujinga wao mkubwa mpaka walipojaribiwa.

▶️ Kuna wengi kanisani ambao wanachukulia kuwa ni kweli kwamba wanaelewa kile wanachokiamini; lakini, hawajui udhaifu wao wenyewe, mpaka dhiki iinuke. Watakapotenganishwa na wale wa imani hiyo na kulazimishwa kusimama wao peke yao kuelezea imani yao, watastaajabishwa kuona mchanganyiko wa mawazo yao juu ya kile walichokikubali kuwa kweli. Kwa hakika ni kwamba kati yetu kumekuwa na hali ya kumuacha Mungu aliye hai na kuwageukia wanadamu, na kutanguliza wanadamu mahali pa hekima ya Mungu.

▶️ Mungu atawainua watu Wake; kama njia nyingine zikishindwa, uasi utakuja miongoni mwao, ambao utawachekecha, ikitenganisha makapi na ngano. Bwana anawaita wote wanaoliamini Neno Lake kuamka kutoka usingizini. Nuru ya thamani imekuja, mahsusi kwa wakati huu. Ni ukweli wa Biblia, ikionesha hatari zilizo mbele yetu. Nuru hii inapaswa kutuongoza kwenye kujifunza Maandiko kwa bidii na uchunguzi muhimu zaidi wa nafasi ambazo tunazishikilia. Mungu angetaka fani zote na nafasi zote za ukweli zichunguzwe vizuri na kwa uvumilivu, kwa maombi na kufunga. Waumini hawapaswi kutulia katika makisio na mawazo yaliyoelezewa vibaya ya kile kifanyacho ukweli. Imani yao sharti iwe na msingi thabiti juu ya Neno la Mungu ili wakati wa majaribu utakapokuja na wakiwa wameletwa mbele ya mabaraza kujibu kuhusiana na imani yao waweze kutoa sababu ya tumaini lile lililo ndani yao, kwa upole na kwa hofu....

🔘 Kwa wale ambao wamejizoeza kuwa walumbanaji kuna hatari kubwa kuwa hawataweza kushughulikia Neno la Mungu kwa haki. Katika kukutana na wapinzani wetu inapaswa kuwa juhudi yetu ya dhati kuwasilisha masomo katika namna ambayo itaamsha ushawishi katika akili zao, badala ya kutafuta tu kumpa ujasiri muumini.
MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA

No comments