VLADIMIR PUTIN AAGIZA OPERESHENI YA KIJESHI NCHINI UKRAINE NA KUYATAKA MAJESHI YA NCHI HIYO KUJISALIMISHA

Putin ametoa tamko hilo katika hotuba ya televisheni huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likimsihi aache.

Katika hotuba yake kwa njia ya Televisheni siku ya Alhamisi asubuhi, Putin anawataka wanajeshi wa Ukraine katika eneo la mapigano mashariki mwa Ukraine kuweka silaha chini na kurejea majumbani mwao.

Aliionya Ukraine kwamba italaumiwa kwa umwagikaji wa damu wowote.

Putin pia anasema "Haki Na Ukweli" ziko upande wa Urusi, akionya kwamba jibu la Moscow litakuwa Lapo Hapo....Ikiwa mtu yeyote atajaribu kuchukua dhidi ya Urusi.

Rais wa Urusi pia anasema hatua za nchi yake ni kujilinda na kuwaambia wanajeshi wa Ukraine baba zao na babu zao hawakupigana ili waweze kuwasaidia Wanazi mamboleo.

No comments