AMKA NA BWANA LEO 24/02/2022

KESHA LA ASUBUHI 

ALHAMISI, FEBRUARI 24 2022

SHERIA YA MUNGU NI KAMILIFU

Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia mjinga hekima. Maagizo ya BWANA ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya BWANA ni safi, Huyatia macho nuru. Zaburi 19:7, 8.

📖 Yesu yule yule, ambaye, alijifunika katika nguzo ya wingu, aliyeongoza majeshi ya Waebrania, ndiye kiongozi wetu. Yeye aliyewapa wana wa Israeli hekima na haki na sheria zilizo nzuri amezungumza nasi kama vile alivyozungumza nao. Mafanikio na furaha yetu hutegemea katika utii wetu usioyumba kwa sheria ya Mungu. Hekima iliyo na ukomo haikuweza kuboresha amri moja ya sheria takatifu. Hakuna hata moja ya amri kumi inayoweza kuvunjwa bila ya kumkosea heshima Mungu wa mbinguni. Kutunza kila nukta ndogo ya sheria ni muhimu kwa furaha yetu wenyewe, na kwa furaha ya wote walioko pamoja nasi. "Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza." Bado viumbe walio na ukomo wataiwasilisha sheria hii takatifu, ya haki, na njema kama nira ya utumwa-nira ambayo hawawezi kuibeba! Ni mkosaji tu ambaye hataona uzuri katika sheria ya Mungu.

📖 Ulimwengu wote utahukumiwa kwa sheria hii. Inafikia hata kwenye dhamira na makusudi ya moyo, na inadai usafi zaidi wa mawazo, shauku, na tabia. Inatutaka sisi kumpenda Mungu sana, na jirani zetu kama tunavyojipenda. Bila kufanyia kazi upendo huu, kauli kuu kukiri imani ni unafiki tu. Mungu anadai, kutoka katika nafsi zote za familia ya mwanadamu, utii kamilifu kwa sheria Yake. "Maana mtu awaye yote atakayeshika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote."

🔘 Kuchepuka kidogo kutoka kwa sheria hiyo, kwa kupuuza, au uasi wa makusudi, ni dhambi, na kila dhambi humweka mwenye dhambi kwenye ghadhabu ya Mungu. Moyo ambao haujafanywa upya utachukia masharti ya sheria ya Mungu, na utajitahidi kutupilia mbali madai yake matakatifu. Ustawi wetu wa milele unategemea uelewa sahihi wa sheria ya Mungu, usadiki wa kina wa tabia yake takatifu, na utii wa hiari kwa matakwa yake. Wanaume na wanawake lazima wasadikishwe juu ya dhambi kabla ya kuhisi hitaji lao la Kristo.... Wale ambao wanaikanyaga sheria ya Mungu chini ya miguuni yao wameikataa njia pekee inayomfafanulia mdhambi kuwa dhambi ni nini. Wanafanya kazi ya mdanganyifu mkuu.
MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA

1 comment: