BENKI YA DUNIA YAMWAGA PESA ZA UJENZI WA UWANJA YANGA
BENKI YA DUNIA YAMWAGA PESA ZA UJENZI WA UWANJA YANGA
Inawezekana huu ndiyo ukawa mwaka wa neema kuliko Miaka yote kwa vinara wa ligi kuu ya NBC Tanzania bara Yanga ambao kwasasa timu hiyo ipo kwenye mikono Salama ya Kampuni ya GSM ambao ndiyo wadhamini wao
Wakati mchakato wa kuendeleza eneo la Yanga kule Kigamboni likiendelea huku Jangwani Neema imefunguliwa na benki ya Dunia kupitia Mradi mkubwa wa Bonde la msimbazi ambao utawahusu klabu ya Yanga na kuwaweka katika mchakato wa kuendeleza eneo lao pale Jangwani
Mradi huo unaotarajiwa kuanza katikati ya mwaka huu umewapa chaguzi mbili klabu ya Yanga Moja kuwajengea Uwanja wa kisasa wenye uwezo wa kuingiza mashabiki elfu 40 na parking za magari na eneo la ofisi za klabu ikiwemo hostels na maduka Chaguzi ya pili ni kuwalipa Pesa ndefu itakayolingana na thamani ya eneo lao
Endapo klabu ya Yanga itakubaliana na moja ya chaguzi hiyo Basi klabu hiyo Itakuwa imeondoka katika matatizo ya kulipia viwanja na hostel za kukodi
Mradi huo mkubwa wa bonde la msimbazi ambao upo chini ya Benki ya Dunia utakuwa ni moja ya kivutio kikubwa sana hapa Jijini Dar es salaam Pindi utakapo kamilika na unatarajiwa kuchukua zaidi ya miaka miwili hadi mitatu ili kukamilika.
Credit Issa Michuzi
Post a Comment