AMKA NA BWANA LEO 11/02/2022

KESHA LA ASUBUHI 

IJUMAA, FEBRUARI 11 2022

FURAHA ILINDWAYO NA SHERIA YA MUNGU 


Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili. Warumi 8:3.

✍🏾 Furaha ya mwanadamu sharti kila wakati ilindwe kwa sheria ya Mungu. Katika kutii pekee ndipo wanapoweza kupata furaha ya kweli. Sheria ni ugo ambao Mungu ameuweka kulizunguka shamba lake la mizabibu. Kwa hiyo wale wanaotii wanalindwa dhidi ya uovu. Katika uasi Adamu alikuwa sheria kwake mwenyewe. Kwa kutokutii aliwekwa chini ya kifungo. Huo ukawa mwanzo wa kutofautiana, kuwa m-binafsi, kuliuingia ubinadamu. Mapenzi yao na mapenzi ya Mungu hayakupatana tena. Adamu alikuwa ameungana na vikosi visivyo na uaminifu, na mapenzi binafsi yakatawala.

✍🏾 Katika Kristo Yesu viwango vya kweli viliwasilishwa. Alifanya iwezekane tena kwa ubinadamu uweze kuunganishwa na Mungu kwa mara nyingine tena. Alikuja kuchukua adhabu ya kifo kwa ajili ya mkosaji. Hakuna hata kanuni moja ya sheria ingeweza kukanyagwa chini ili kuwakaribia wanaume na wanawake katika hali ya kuanguka kwao; kwa hiyo Yesu Kristo alitoa maisha Yake kwa ajili yao, kuteseka kwa niaba ya adhabu ya kutokutii kwao. Hii ilikuwa ndiyo njia pekee ambayo kwayo ubinadamu ungeweza kuokolewa, njia pekee ambayo ingeweza kudhihirishwa kuwa inawezekana kwao kutunza sheria. Yesu Kristo alikuja katika dunia hii na alisimama mahali ambapo Adamu alisimama, akishinda pale ambapo Adamu alishindwa kushinda. Alifanyika kwetu hekima na haki na utakaso na ukombozi....

🔘 Kabla ya kuwekwa msingi wa ulimwengu, aliahidi kwa neno Lake kwamba angeyatoa maisha Yake kama fidia ikiwa wanaume kwa wanawake wangegeuka kutoka katika kuonesha utii wao kwa Mungu. Alifunua upendo wake kwa kujinyenyekesha Mwenyewe, akijishusha kutoka mbinguni ili kufanya kazi kati ya wanadamu walioanguka, wasio na utaratibu, na wasio na sheria. Kwao wenyewe hawangeweza kukabiliana na adui. Yesu Kristo alijitoa mwenyewe na kila alichokuwa nacho, utukufu Wake, tabia Yake, kwa ajili ya kuwahudumia wale wanaorejesha uaminifu wao na kutunza sheria ya Mungu. Hili ndilo tumaini lao pekee. Kristo anasema waziwazi, sikuja kutangua sheria. Ni nakala ya tabia ya Mungu, na nilikuja kutekeleza kila uhalisia wake. Nilikuja kuithibitisha kwa kuiishi katika namna ya mwanadamu, kuonesha mfano wa utii mkamilifu.
MUNGU AKUBARIKI SANA

No comments