SIKU YA MAOMBI LEO 09/01/2022
*SIKU KUMI ZA MAOMBI 2022.*
Jumapili, 09/01/2022.
*SOMO: MTINDO WA MAISHA YA UTII NA MAOMBI.*
*Fungu elekezi:14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba. 1 Yohana 5:14-15.*
Hatuna Uwezo, Lakini Yeye ni Mwenye Uweza. Wote.
Ujumbe wa malaika watatu unatutaka tuishi Maisha ya utii. Malaika wa kwanza anasema kuwa, “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake
imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” (Ufunuo 14:7). Agano Jipya liliandikwa kwa lugha ya Kiyunani, na neno ‘Mcheni’
lililotumika katika aya hii, linaweza pia kutafsiriwa kama heshima, uchaji, au stahi sana. “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri
zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila
kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.” (Muhubiri 12:13, 14)
Tunapofikiria kuhusu kushika amri za Mungu, ni rahisi sana kujielekeza katika udhaifu wetu, mapungufu yetu, na ukosefu wetu wa uwezo wa kufanya kile ambacho ndani yetu tunatamani kukifanya. Mara nyingi tunatamani kutenda mema, lakini tunashindwa kupata nguvu na uwezo wa kutimiza matamanio yetu. Hapo ndipo tunapoungana na Mtume Paulo kutambua kuwa, “… sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.” (Warumi 7:15). Ufumbuzi wa mtume kwa
changamoto hii ulikuwa ni upi? Na mwisho wa sura hiyo anauliza swali kuwa, “Ole
wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru
Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.” (Warumi 7:24, 25). Kuna ufumbuzi kwa tatizo ambalo daima linatuangusha, tunatubu, na
kuangauka tena. Paulo anasema kuwa, ufumbuzi ni Yesu Kristo Bwana wetu. Sisi ni wadhaifu, lakini yeye ni mwenye nguvu. Sisi ni dhaifu, lakini yeye ni mwenye uweza mkuu. Hatuna nguvu, lakini yeye anazo nguvu zote. Ellen G. Whita anaweka kwa namna ya kuvutia katika Makala yake aliyoandika mwaka 1897 kuwa:
*“Mfano wa Yesu unatuonesha kwamba tumaini letu pekee la ushindi ni kuendelea kupinga mashambulizi ya Shetani. Yeye aliyemshinda adui wa roho katika pambano lenye majaribu, anafahamu uwezo wa Shetani dhidi ya ubinadamu, na ameshinda kwa niaba yetu. Yeye kama mshindi ametupatia faida ya ushindi wake, ili kwa jitihada zetu tupinge majaribu ya Shetani tukiunganisha udhaifu wetu na nguvu zake, kutokustahili kwetu na kustahili kwake. Na katika kufanya hivyo, tutegemezwe kwa uwezo wake unaostahimili chini ya majaribu makuu, tuweze kumpinga adui kwa uwezo wa jina lake lenye nguvu kama yeye mwenyewe alivyoshinda. Signs of the Times, May 27, 1887.*
*Kudai Ushindi.*
Tulikuwa washindi katika Maisha ya Kikristo pale tulipojielekeza katika uwezo wa
Kristo, tukisahau udhaifu wetu. Kadiri tunavyoingia katika maombi, hebu na tudai ahadi
iliyoko katika 1 Yohana 5:14, 15 “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba
kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho
chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba” Kadiri tunavyodai ahadi hii kwa
uaminifu, Yesu atatenda mambo makubwa ya kushangaza, na kutuimarisha ili kuweza
kuishi Maisha ya kimbingu wakati tukijitayarisha kwa kurudi kwake mara ya pili
ambako kumekaribia.
Wakati wa Maombi (Dakika 30-45)
Kuomba kupitia kwa Neno la Mungu – Mhubiri 12:13, 14.
“Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri
zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila
kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.”
*“Mcheni Mungu”*
Bwana, tunatambua kwamba wewe ndiye Mungu Muumba mwenye uwezo, mwenye
maarifa yote. Wewe umezidi upeo wa mwanadamu wa utambuzi, lakini bado upo karibu
nasi kuliko hata wapendwa wetu wanaoonekana kuwa karibu. Tupo chini ya utisho wa
ukuu wako na tunakuabudu wewe tukikusudia kukuheshimu katika Maisha yetu.
*“Shika Amri Zake.”*
Ee Mungu, sisi hatuna uwezo ndani yetu wa kushika amri zako, wa kuenenda sawa sawa
na mapenzi yako. Ni Yesu pekee anayeweza kutusaidia. Tunatamani kutenda mapenzi
yako, kuwa waaminifu, lakini mara nyingi tumeshindwa. Ahsante sana kwamba Yesu
anao uwezo wa kuleta ushindi katika Maisha yetu. Tunamgeukia na kujitoa kikamilifu
katika mikono yake ya uaminifu. Ee Yesu, tunaomba kwamba uishi Maisha yako ndani yetu.
*“Kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.”*
Baba, ninatambua kwamba hakuna jambo lililofichika mbele yako. Unaufahamu moyo
wangu, unafahamu mapito yangu. Unatambua fika kila kitu kinachotokea katika
ulimwengu unaonizunguka. Ahsante sana kwamba, pamoja na jinsi ninavyojisikia,
unaniwazia kwa upendo na neema, na sina hofu na hukumu kadiri ninavyodumu ndani ya Yesu.
*Mapendekezo zaidi ya Maombi.*
Shukurani na Sifa: Shukuru kwa mibaraka mahususi na msifu Mungu kwa wema wake.
Kuungama: Tumia dakika chache kwa ajili ya maungamo binafsi na msifu Mungu kwa
msamaha wake.
Uongozi: Mwombe Mungu akupatie hekima kwa changamoto na maamuzi ya sasa.
Kanisa Letu: Muombe Mungu kwa ajili ya mahitaji ya kanisa katika ngazi ya majimbo
na kanisa la ulimwengu (tazama karatasi nyingine yenye mahitaji).
Mahitaji ya eneo mahalia: Ombea mahitaji ya washiriki wa kanisa, familia, na majirani.
Sikiliza na Itika: Tumia muda kuisikiliza sauti ya Mungu na kuitikia kwa sifa au wimbo.
Mapendekezo ya Nyimbo.
Yote Namtolea Yesu (#122)
Nitembee Nawe (#14)
Ni Wako Bwana (#144)
Njiani Huniongoza (#155)
Wimbi Litakasalao (#188)
*MUNGU ATUBARIKI SOTE KWA KUPITIA MAOMBI TUNAYOOMBA.*
Post a Comment