AMKA NA BWANA LEO 09/01/2022
Jumapili 09/01/2022
*USIOMBE TU, LAKINI OMBA NA UFANYE KAZI!*
*Ndipo mfalme akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni. Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vyema,... Tafadhali unipeleke mpaka Yuda, niuendee mji wa makaburı ya baba zangu, nipate kuujenga.* *Nehemia 2:4,5*
*Wakati Nehemia akisihi kwa ajili ya msaada wa Mungu, hakukunja mikono yake, akihisi kuwa hana cha kufanya zaidi au wajibu katika kulieleza wazi lengo lake la kuujenga Yerusalemu. Kwa busara na mawazo ya kupendeza aliendelea kufanya mipangilio yote muhimu kuhakikisha mafanikio ya jambo hilo*.
Mfano wa huyu mtu mtakatifu unapaswa kuwa somo kwa watu wote wa Mungu, kwamba hawapaswi tu kuomba kwa imani, lakini pia kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu. Je, ni mambo magumu kiasi gani tunayokutana nayo, ni mara ngapi tunazuia utendaji kazi wa Mungu kwa niaba yetu, kwa sababu busara, kuona mbali, na bidii ya kazi yanachukuliwa kama yasiyohitajika sana katika dini! Hili ni kosa kubwa sana. *Ni wajibu wetu kuendeleza na kutumia kila nguvu ambayo itatupatia watenda kazi bora zaidi kwa Mungu. Upembuzi yakinifu na mipango iliyopangwa vizuri ni vya muhimu katika mafanikio ya mambo matakatifu leo kama vile ilivyokuwa katika nyakati za Nehemia.*
*Wanaume na wanawake wa maombi yapasa wawe wanaume na wanawake walio watendaji*. Wale walio tayari na wanaotaka watapata njia na namna ya kufanya kazi. *Nehemia hakutegemea mashaka*. Vitu ambavyo hakuwa navyo aliomba kutoka kwa wale ambao waliweza kutoa.
*Bwana bado anafikia mioyo ya wafalme na watawala kwa niaba ya watu Wake. Wale wanaofanya kazi kwa ajili Yake wanapaswa kufaidika kwa msaada anaowahamasisha wanaume na wanawake kutoa kwa ajili ya mafanikio ya kazi Yake.* *Mawakala ambao kupitia kwao karama hizi zinatolewa wanaweza kufungua njia ambayo kwayo nuru ya ukweli itatolewa kwa maeneo mengi yasiyo na nuru.* Watu hawa wanaweza kuwa watu wasio na huruma na kazi ya Mungu, wala imani kwa Kristo, wala uzoefu wa Neno Lake; lakini hii sio sababu ya kukataliwa kwa matoleo yao.
*Bwana ameweka mali zake katika mikono ya wasioamini pamoja na wanaoamini; wote wanaweza kumrudishia Yeye mwenyewe kwa ajili ya kufanya kazi hiyo kwa ulimwengu ulioanguka. Ilihali tungalipo katika dunia hii, ilimradi Roho wa Mungu anashughulikia mioyo ya wanadamu, tutapokea neema na kuwapatia wengine.*
*MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*
Post a Comment