PROF. MAKUBI AZITAKA TAASISI KUUNGA MKONO UHAMASISHAJI WA CHANJO ZA COVID-19
Katibu Mkuu wa Wizara ya afya Prof. Abel Makubi amezitaka taasisi zote ambazo ziko chini ya Wizara hiyo kuunganisha nguvu katika kampeni shirikishi na harakishi ya uhamasishaji wa chanjo dhidi ya UVIKO-19 ili wananchi waweze kuhamasika kuchanja zaidi na kufikia malengo waliyojiwekea.
Prof. Makubi ametoa wito huo wakati wa kikao kazi kilichohusisha wakurugenzi kutoka taasisi mbalimbali ambazo ziko chini ya Wizara ya afya kilichofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Prof. Makubi amesema hadi sasa wanachi waliopata chanjo ya UVIKO-19 wamefikia asilimia 3.3.
Katika kikao hicho Katibu Mkuu ameweza kuwapitisha wakurugenzi katika maeneo ya vipaumbele vya wizara takriban kumi ikiwemo uboreshaji wa huduma za afya,bidhaa za dawa, UVIKO-19, Uongozi, Bima ya afya kwa wote, vifo vya mama na mtoto, Magonjwa ya kuambukiza (NCDs), huduma za kibingwa na bobezi, miundombinu na vifaa, watumishi, tehama na takwimu pamoja na tafiti.

Post a Comment